Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitangaza kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete eneo la Soweto
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na Nape namna matembezi yatakavyoanza
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungiamikono wananchi kabla ya matembezi kuanza
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwapungia mkono wananchi matembezi
yalipoanza eneo la Soweto. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Kinana
na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi hayo huku
akiwa na watoto ambao aliwateua kutembea nao baada ya kuwaona eneo la
Soweto
"Haya Simameni Hapa tutembee wote" Rais Jakaya Kikwete akiwaambia watoto hao kabla ya kuanza matembezi
"Vipi Mmechoka", Rais Kikwete akiwauliza watoto, lakini wakasema
hawajachoka ambapo walitembe hadi mwisho umbali wa kilometa tano
Rais Kikwete akiongoza matembezi hayo
Wakazi wa Mbeya wakiwa katika shamrashamra za matembezi hayo
Wafanyabiashara katika soko lililopo karibu na Uwanja wa
Sokoine,wakimpungia mkono Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete wakati akipita
eneo hilo wakati wa matembezi hayo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasli kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine yalikokomea matembezi hayo
Wana-CCM na wananchi kwa jumla wakimlaki Rais Kikwete kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wakati
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete alipowasili kwenye Bustani ya Uwanja wa
Sokoine mwishoni mwa matembezi hayo
Mbunge wa Kyela, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimia wananchi mwishoni mwa matembezi hayo
Mbunge wa Rungwe Mashariki,Profesa Mark Mwandosya akikaribishwa na Nape
kusalimia wananchi mwishoni mwa matembezi hayo, ambapo alisema afya
yale imeimarika hasa baada ya kuonyesha uwezo wa kushiriki matembezi
hayo ya kilometa tano mwanzo hadi mwisho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa amepumzika na viongozi
wenzake baada ya kuwasili kwenye bustani ya Uwanja wa Sokoine mjini
Mbeya baada ya matembezi hayo
Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda akisalimiawananchi baada ya matembezi hayo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia mwishoni mwa matembezi hayo
Mangula akisalimia mwishoni mwa matembezi hayo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akihitimisha matembezi kwa kuwasilimia wananchi baada ya matembezi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Naibu
wake (Bara) Mwigulu Nchemba wakati wakimsubiri Mwenyekiti wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete kuwasili eneola Soweto kuanza matembezi ya mshikamano
kuadhimisha miaka 37 ya CCM, leo mjini Mbeya
Katibu wa NEC, Ogamaizesheni Mohamed Seif Khatib, Katibu wa NEC Uchumi
na Fedha Zakiah Megjj na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania,
Abdallah Bulembo wakibadilishana mawazo wakati wakimsubiri Jk eneo la
Soweto kuanza matembezi hayo
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwigulu na Katibu Mkuu
wa UVCCM, Sixtus Mapunda wakibadilishana mawazo eneo la Soweto kabla ya
matembezi kuanza
Mkazi wa Mtaa wa Soweto jijini Mbeya akijimwayamwaya wakati akisubiriwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuanza matemebezi hayo
Wana-CCM wakiselebuka wakati wakimsubiri Mweneyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuwasili eneo la Soweto
Picha zote na theNkoromo Blog
0 comments:
Post a Comment