SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, February 12, 2014

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Yaamuru Jengo Lenye Ghorofa 18 Karibu na IKULU Lipunguzwe Urefu Kwanzia Ghorofa ya Saba Kwenda Juu.

Vigogo wa TBA, Makumba Kimweri (kulia) na Richard Maliyaga (kushoto) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar!.Picha na Maktaba
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu, Richard Maliyaga, kila mmoja kulipa faini ya Sh15 milioni au kwenda jela miaka tisa baada ya kuwatia hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuruhusu ujenzi wa jengo la ghorofa 18 karibu na Ikulu.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo alisema jengo hilo lilipaswa kuwa la ghorofa sita na kuamuru kubomolewa kuanzia ghorofa ya saba kwenda juu.
Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......

0 comments:

Post a Comment