Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI),
Ramadhani Madabida (kulia) na Ofisa Ubora wa Bidhaa wa Bohari Kuu ya
Dawa (MSD), Evance Mwemezi walipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana kusomewa mashtaka ya kuuza na kusambaza
dawa feki za ARV. Picha na Venance Nestory
--
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Ltd cha Dar es
Salaam (TPI), Ramadhani Madabida na wenzake watano wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo
la kusambaza dawa bandia na kusababisha hasara ya Sh148.3 milioni.
Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi aliwataja
washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo kuwa ni Mkurugenzi wa
Operesheni wa TPI, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msofe, Mhasibu
Msaidizi, Fatma Shango pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD),
Sadick Materu na Evans Mwemezi.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......
0 comments:
Post a Comment