Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalenga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Iringa vijijini Pudensiana Kisaka.
Godfrey Mgimwa; Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM
---
PINGAMIZI lililowekwa
na Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace
Tendega dhidi ya Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Godfrey Mgimwa
limetupiliwa mbali.
Mgimwa amewekewa pingamizi hilo kwamba sio raia wa Tanzania na kwamba watu waliomdhamini hawatokei jimbo la Kalenga.
Msimamizi
wa uchaguzi wa jimbo la Kalenga, Pudensiana Kisaka alisema tume hiyo
iliamua kuruhusu kampeni ziendelee baada ya upande wa walalamika
kujishindwa kupeleka vielelezo.
Alisema
baada ya kupata pingamizi hilo, tume iliagiza pande zote mbili,
kupeleka vielelezo vyake ili kujiridhisha na pingamizi hilo.
Hata
hivyo chadema, walishindwa kupeleka uthibitisho wa pingamizi lao kwa
muda ulipangwa na badala yake, walipeleka barua ya kusisitiza pingamizi
hilo.
Katibu
wa CCM, wilayani Iringa Amina Imbo alisema mgombea wake ni raia wa
kuzaliwa wa Tanzania na kwamba, pingamizi hilo halina maana na kamwe
halitaweza kuvuruga kampeni za chama hicho.
Imbo
aliongeza kuwa CCM ilisimamia kikamilifu kuhakikisha, fomu za mgombea
zidhaminiwa na wananchi wa jimbo husika ambao waliambatanisha shahada za
kupigia kura kutoka jimboni na si vinginevyo.
Mgimwa
amezaliwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa, amesoma shule ya msingi
wilolesi na baadae kujiunga na shule ya sekondari ya Njombe (NJOSS),
kabla ya kwenda jijini na Dar es salaan kisha nchini uingereza kwa
masomo yake ya elimu ya juu.
Anayo
passport ya kusafiria inayoonyesha kwamba ni raia wa Tanzania wa
kuzaliwa na cheti cha kuzaliwa na hajawahi kukataa utanzania.
0 comments:
Post a Comment