Dk Mohammed Hafidh Khalfan
mmoja wa wanabodi wa PBZ alipokuwa akitoa nasaha zake wakati wa ufunguzi
wa makao makuu ya Benki ya Kiislamu, Mpirani.
I. Shukran
a. Kwa Allah.
b. Mgeni rasmi
c. Waalikwa wote na ambao
wanafuatilia uzinduzi huu. Kadhalika, waliofanikisha uanzishwaji wa
huduma hizi za kifedha kwa mfumo wa Kiislam.
2. Kazi kubwa imefanywa na Serikali yetu
ya Zanzibar kuamua kuwa mwanzilishi wa huduma hizi hapa nchini. Inataka
ujasiri kutoa huduma mpya ukiwa hujui kama utafanikiwa au laa.
Lilofanywa na SMZ ni kutoa mhanga kitoto
chake hicho hicho kimoja kama alivyofanya Nabii Ibrahim 'Alayhis
Salaam. kwa mwanawe pekee Ismail 'Alayhis Salaam. Na matokeo ya kuwa
tayari kutoa au kufanya kwa ajili ya Aliyetuumba Akaturuzuku ni
mafanikio yasiyo shaka. Na tumeanza kuyaona kwa kuongezeka mtaji, idadi
ya wateja na kukua uchumi wetu.
Benki ya Kiislam bila ya bima ya Kiislam
huwa haijakamilika. Hilo ni ombi letu kwa Serikali yetu sikivu kwa
mahitaji ya raiya wake.
3. Nihitimishe kwa kukumbusha kuwa
huduma za kifedha zinazofuata Sharia ni nyingi. Nyengine kama vile Sukuk
(Islamic Bonds) zimesaidia chumi nyingi duniani hata ambazo wakazi wake
wengi si Waislam.
Tusichelewe zaidi, ikiwa Uingereza
imejikubalisha kuwa International Islamic Financial Hub kwanini Zanzibar
isiwe East African Islamic Financial Hub? Linawezekana pindi
tukidhamiria.
Tunaomba katika hili Serikali ikishirikiana na Sekta Binafsi walifanyie kazi kwa dhati na haraka.
Ahsanteni
HABARI NA ZANZINEWS.COM
0 comments:
Post a Comment