Waziri
wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63)
enzi za uhai wake
Rais Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue
----
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa
za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa
Jimbo la Kalenga (Mkoa wa Iringa) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza
Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango
wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na
mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
Kifo cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana
wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi
Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa
Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati)
katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic , Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa
amelazwa kwa muda sasa.
Balozi Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha
nyumbani mwili wa Waziri Mgimwa yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na
familia yake na kuwa taarifa zaidi za suala hilo zitatolewa baadaye kwa
kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea.
--
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo
la Kalenga akisema kuwa wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi
yao.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa
mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa
William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa Jimbo la Kalenga (Mkoa wa
Iringa) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
Kifo cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati) katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic , Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa amelazwa kwa muda sasa.
Balozi Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Waziri Mgimwayanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake na kuwa taarifa zaidi kuhusu suala hilo zitatolewa baadaye kwa kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea.
Katika salamu zake kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na kwa familia ya Marehemu Mgimwa, Rais Kikwete amesema: “Sina maneno ya kutosha kuelezea mshtuko na huzuni yangu kubwa kufuatia taarifa za kifo cha Mheshimiwa Mgimwa. Binafsi nimemtembelea mara mbili kwenye Hospitali alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia yake na tamaa yake ya kurejea nyumbani kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.”
Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Sote tunajua mchango wake katika Serikali. Sote tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya ni mapenzi ya Mungu.”
“Napenda kutoa pole nyingi na rambirambi zangu za dhati kwa wana-familia wote kwa kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi katika kuomboleza msiba huo mkubwa. Napenda mjue kuwa msiba huu ni msiba wangu pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,” amesema Rais Kikwete.
Rais pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo la Kalenga akisema kuwa wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi yao.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
01 Januari, 2014
Salutation | Honourable | |
First Name: | William | |
Middle Name: | Augustao | |
Last Name: | Mgimwa | |
Member Type: | Constituency Member | |
Constituent: | Kalenga | |
Political Party: | CCM | |
Member Status: | Current Member | |
Date of Birth | 20 January 1950 |
EDUCATION
|
||||
---|---|---|---|---|
Start Date | End Date | Level | ||
Institute of Development Management, IDM, Mzumbe | MBA (Finance) | 1989 | 1991 | MASTERS DEGREE |
Institute of Finance Management, IFM | Postgraduate (Finance) | 1983 | 1984 | POSTGRADUATE |
Institute of Finance Management, IFM | Advanced Diploma (Banking) | 1975 | 1978 | ADV DIPLOMA |
Tosamaganga Seminary School | O-Level Education | 1968 | 1969 | SECONDARY |
Mafinga Seminary School | O-Level Education | 1970 | 1971 | SECONDARY |
Wasa Primary School | Primary Education | 1961 | 1965 | PRIMARY |
Tosa Seminary Primary School | Primary Education | 1966 | 1967 | PRIMARY |
EMPLOYMENT HISTORY
|
|||
---|---|---|---|
Company Name | Position | From | To |
The Parliament of Tanzania | Member - Kalenga Constituency | 2010 | 2015 |
Bank of Tanzania Training Institute (Mwanza) | Principal | 2000 | 2010 |
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank | Director | 1997 | 2000 |
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank | Manager | 1996 | 1997 |
The National Bank of Commerce (NBC) - College | Lecturer | 1981 | 1989 |
The National Bank of Commerce (NBC) - Bank | Accountant | 1980 | 1981 |
Ministry/Political Party/Location | Position | From | To |
---|---|---|---|
Chama Cha Mapinduzi, CCM | Ward Guardian (Wasa, Iringa) | 2008 | 2010 |
Chama Cha Mapinduzi, CCM | Assistant Commander (UVCCM) | 1994 | 1995 |
Chama Cha Mapinduzi, CCM | Councillor (Gangilonga Ward) | 1991 | 1994 |
PUBLICATIONS | |
---|---|
Description
|
Date |
W. Mgimwa: Liquidity Management, Tanzania Bankers Journal, Dar Es Salaam. | 1994 |
W. Mgimwa: Commercial Bank Lending Journal, Dar Es Salaam. | 1995 |
W. Mgimwa: Advanced Credit Operations, Dar Es Salaam. | 2007 |
W. Mgimwa: Advanced Treasury Management, Dar Es Salaam. | 2009 |
0 comments:
Post a Comment