SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, January 30, 2014

Mwenyekiti wa Chadema, Katibu Mkuu wa Chadema,Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa Walivyotua na Chopa Mkoani iringa,Kijiji cha Kigonzile mji wa Ifunda na Kuzindua Operesheni(M4C)Pamoja Daima Maelfu Wajitokeza

   Chopa ya Chadema ikitua na viongozi wakuu wa Chadema uwanja wa Mwembetogwa
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa akiwasili katika  kiwanja cha Mwembetogwa
 Slaa Iringa; Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Iringa, katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa jana
  Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwahutubia wana Iringa 
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa mjini Iringa jana.
 Katibu  mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Dr Slaa akimpokea kada wa CCM ambae amehamia  Chadema leo ,kulia ni kata wa TLP Bw  Samson
 Dr Slaa akimpokea kada wa  TLP Bw Samson Mrisho ambae amejiunga na Chadema leo uwanja wa Mwembetogwa
 Mgombea wa udiwani katika Kata ya Nduli mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ayoub Mwenda akijinadi mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, uliofanyika kijijini hapo jana.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowen akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Kigonzile katika Kata ya Nduli mkoani Iringa, baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima jana
 Mbunge wa Kawe, Haliama Mdee (Chadema), akiwahutubia wananchi wa mji wa Ifunda, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, akiwahutubia wanachi wa mji wa Ifunda mkoani Iringa, katka mkutano wa OperesheniM4C Pamoja Daima juzi.
 Maelefu ya wakazi wa Manispaa ya Iringa na vitongoji vyake wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesheni ya M4C Pamoja Daima wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa jana.Picha na Chadema

0 comments:

Post a Comment