Gari maalum lililobeba mwili wa Marehemu Mzee Nelson Mandela likitokea Hospitalini na msafara kuelekea sehemu maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya watu maarufu kutoa heshima za mwisho.
Raia wa Afrika Kusini wakiwa wamejipanga kando kando ya barabara kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Nelson Mandela.
Mwili wa Mzee Nelson Mandela ukiwasili kwenye jengo lililopo mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria, ambapo utalala kwa siku tatu kuruhusu Raia wote wa Afrika Kusini na Dunia kwa ujumla kutoa heshima zao za mwisho.
Mwanamindo wa Kimataifa Naomi Campbell alishindwa kuzuia hisia zake baada ya kuona jeneza la Mzee Nelson Mandela likiwasili kwenye viwanja hivyo tayari kwa kutoa heshima za mwisho.
Naomi Campbell akionekana kutoa amini kwa kile alichokiona.
Mzee Nelson Mandela enzi za uhai wake alikuwa akimpenda Mwanadada huyu na kumuona kama mjukuuu wake.
Bono akitoka kutoa heshima zake za mwisho kwa mzee Nelson Mandela huku akiwa maembatana na Mkewe Ali Hewson (left) pmoja na aliyekuwa msaidizi wa Mzee Mandela Zelda le Grange.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiwa ameongozana na wajane wa Mzee Nelson Mandela kwenda kutoa heshima za mwisho kwenye sehemu maalum iliyoandaliwa.
Mke wa kwanza wa Mzee Nelson Mandela akionekana na majonzi mazito akielekea kutoa heshima za mwisho kwa mumewe wa zamani.
Rais Jacob Zuma na mkewe wakitoa heshima za mwisho.
Gaazeti la Daily Mail kwenye picha hii ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wamemuita “Dikteta” kutokana na uchu wake wa madaraka hadi leo.
Raia wa Afrika Kusini wakiwa wamejipanga kando kando ya Barabara kwa ajili ya kutoa heshima zao huku wakiimba na kusifu juhudi za Mzee Nelson Mandela kupigania Uhuru wa nchi yao.
0 comments:
Post a Comment