SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, December 22, 2013

MANJI AWAOMBA WANACHAMA WA YANGA WASIVUNJIKE MOYO

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
 
MANJI AKUBALI KIPIGO CHA 3-1
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amekubali kipigo cha 3-1 kutoka kwa Simba na kusema asitupiwe lawama mchezaji wala kiongozi yeyote kwa matokeo ya jana.
Manji ameyasema hayo leo wakati akiongea na wanahabari katika makao makuu ya timu yake yaliyopo  Mtaa wa Twiga na Jangwani baada ya mechi ya jana ya Watani wa Jadi, Simba na Yanga, kwenye mchezo wa ‘Nani Mtani Jembe’ uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Manji ameongeza kuwa kama ni lawama basi alaumiwe yeye maana ndiye kiongozi wa timu.
 
HABARI NA GPL
 

 
 Imeandikwa Na  Mjengwa Blog
Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji.
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.

0 comments:

Post a Comment