SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, December 22, 2013

BENKI YA KCB TANZANIA YAMWAGA MISAADA JIJINI‏

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir (wa pili toka kulia) akimkabidhi msaada wa Mashine ya kupasha moto vifaa vya hospitali kabla ya matumizi na baada ya matumizi  kwa mgonjwa (Sterilizer) Mkurugenzi wa Zahanati ya Njia Heath Centre ya Kiwalani jijini Dar es Salaam, Bw. Stephen Mosha (wa pili toka kushoto). Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vyote vyenye thamani ya  shilingi milioni 5, wengine wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi. Hellen Olengailuva na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya hiyo  Christina Manyenye.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye, akimkabidhi Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mabati na saruji  vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 2. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata jijijini Dar es Salaam. Msaada huo utamsaidia kwa ajili ya ukarabati wa nyumba yake.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye akimkabidhi  Mwishehe Saidi ambaye ni mlemavu msaada wa mifuko ya  Saruji 28, Mabati 18 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 2. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mwishehe Tabata jijijini Dar es Salaam. Msaada huo utamsaidia kwa ajili ya ukarabati wa nyumba yake.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano  wa benki ya KCB Tanzania, akisoma hutuba kwa wakazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa benki  hiyo walipofika kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 katika Zahanati ya NJia  Health Centre. Anayeshuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Moezz Mir.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Njia  Health Centre, Bw. Stephen Mosha wakati walipofika katika kituo hicho kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam,kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5. Katikati ni Mkuu wa Utawala wa kituo hicho Bi. Hellen Olengailuva.  
Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Njia Heath Centre kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam, Bw. Stephen Mosha, akiongea na waandishi wa habari wakati  Uongozi wa Benki ya KCB Tanzania, walipofika Hospitalini hapo kutoa  msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya shilingi Milioni 5. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki  hiyo Bw. Moezz Mir na Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Christina Manyenye.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya KCB Tanzania wakiwa katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali katika kituo cha Afya cha Njia Health Centre Kiwalani jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 vilitolewa na benki hiyo.

0 comments:

Post a Comment