Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela atazikwa Jumapili ya tarehe 15 ya mwezi huu wa Disemba, katika kijiji cha Qunu. Taarifa hizo zimetangazwa jana na Rais Jacob Zuma ambapo amesema wiki nzima ya maombolezo itahusisha ibada na shughuli ya kuuaga mwili itakayofanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Johannesburg. Aidha, Jumapili itakuwa siku ya maombi kitaifa na kisha mazishi ya Mandela yatafanyika kitaifa mjini Pretoria kuanzia Jumatano hadi Ijumaa. Mwili wa Mandela jana umepelekwa katika hospitali ya kijeshi, Pretoria. Mandela amefariki dunia juzi usiku akiwa na umri wa miaka 95.
Saturday, December 7, 2013
Mandela Kuzikwa Disemba 15
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, December 07, 2013
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
Mandela kuzikwa Disemba 15
0 comments:
Post a Comment