Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika
mahafali ya kwanza ya shule ya Awali ya Istiqaama iliyopo Majumbasita
katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Katika hotuba yake hiyo
aliwaasa waislamu kuwaendeleza watoto wao kielimu katika taasisi za
kidini zilizopo ili waweze kupata elimu zote za kitaaluma na kidini
waweze kuwa na ujuzi na maadili mema. Aliwataka pia Waislamu kujenga
tabia ya kuchangia taasisi zao ili ziweze kusonga mbele katika malengo
waliojiwekea. Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga Ndugu Adam Misana.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shule ya Istiqaama English Medium and Primary School ya
Sumbawanga Amr Said akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza katika mahafali
hayo. Katika risala iliyosomwa kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala
Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima Shule hiyo ilianza rasmi
Januari mwaka huu 2013 ikiwa na wanafunzi 48 na hidi hivi sasa ina
wanafunzi 6. Shule hiyo inayoendeshwa na taasisi ya kidini ya ISTIQAAMA
ina mpango wa kujenga shule ya msingi katika kipindi cha mwaka 2014-2017
na shule ya Sekondari katika kipindi cha mwaka 2018-2021.
Zoezi la utoaji wa vyeti kwa wahitimu
Wahitimu wa kike
Wahitimu wakiumeni
Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo, kushoto kwao waliketi wanawake.
Baadhi
ya watoto wakiwa wanacheza katika moja ya sehemu za michezo katika
shule hiyo. Pichani nyuma ni sehemu ya madarasa ya shule hiyo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
0 comments:
Post a Comment