Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa
----
Polisi mkoani Kigoma, imemshauri, Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa
kusitisha ziara zake mkoani Kigoma kwa sababu za kiusalama.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia
Makunja alisema jana: “Ni ushauri tu tunatoa kwa Dk Slaa kwamba anaweza
kuahirisha kutokana na hali ilivyo hapa.” Hata hivyo, Kamanda Makunja
alisema pamoja na yote hayo bado Polisi mkoani, Kigoma imejipanga imara
kukabiliana na vurugu zozote zinazoweza kutokea katika ziara hiyo.
Lakini Dk Slaa alipoulizwa kuhusu ushauri huo
alisema hawezi kufuta ziara hiyo na kusema hahofii chochote. Alisema na
alishafahamu siku nyingi kuwa hayo yanayotokea. Juzi, vijana mbalimbali
waliandamana kwa pikipiki na wengine wakitembea kwa mguu huku wakiwa na
mabango kupinga ziara ya Dk Slaa Kigoma. Anatarajiwa kuwasili Kigoma
Kaskazini keshokutwa.
Hatua hiyo ya kupinga ziara hiyo, imetokana na
Kamati Kuu ya Chadema kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Chadema, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.........
0 comments:
Post a Comment