Aliyekua Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Ananilea Nkya
****
Dr Kitila, Mwigamba na mwanangu
Zitto,
Niwape ushauri
kidogo.
Kama kweli haya tuliyoelezwa mmehusika, ni vema
mkakubali kwamba kuna mahala mmepotoka kiasi. Sisi tunatambua kuwa binadamu
huweza kukosea ili mradi mtu asifanye makosa kwa kukusudia. Adhabu
iliyotolewa kwenu kuvuliwa vyeo, nionavyo mimi utaratibu wa kibinadamu wa
kurekebishana.Kama kweli mnahusika kwa chembe katika haya, na kama kweli
hamjanunuliwa kuvuruga nia njema ya kujenga upinzani imara wa kisiasa nchini
kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla, basi msiwe
na papara.
Tulieni tafakarini na kisha ombeni radhi. Ninaamini
mkifanya hivyo, uongozi wa chama chenu,wanachama na Watanzania watawasamehe na
kisha rudini kazini jengeni chama chenu kiweze kuimarika zaidi kwa ajili ya
kuwatumikia Watanzania kwa umakini, uaminifu na ujasiri usiotiliwa
shaka.
Mkifanya hivyo mtajenga utaduni mpya wa kuigwa nchini
na wanasiasana heshima yenu itapanda juu. Mkifanya vinginevyo, mnaweza
mkaonekana mliingia CHADEMA kwa lengo la kuvuruga au kutafuta umaarufu, fedha
au vyeo haraka haraka.
Mungu awabariki.
Ananilea
Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo. com
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.
NA HAKINGOWI
0 comments:
Post a Comment