Askari
wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakishusha kwenye gari jeneza
lenye mwili wa askari mwenzao, marehemu Luteni Rajab Mlima wakati wa
maziko yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam jana
jioni Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda
Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima Gavana eneo la Goma.
Askari
wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakiwa wameinamia kwa huzuni
jeneza lenye mwili wa askari mwenzao, marehemu Luteni Rajab Mlima
wakati wa maziko yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu, Dar es
Salaam jioni hii. Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa Mataifa
la Kulinda Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima Gavana eneo
la Goma.
Waombolezaji wakijiandaa kufanya maziko
Waombolezaji wakifanya maziko
===
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakifyatua risasi juu kama ishara ya heshima kwa marehemu Luteni Rajabu Ahmed Mlima katika shughuli za maziko kwa mujibu wa taratibu za Kijeshi.
Meja Leonidas Benedict Luangisa akisoma wasifu wa marehemu.
====.
Hussein Makame, MAELEZO
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha ameongoza maziko ya marehemu Luteni Rajabu Ahmed Mlima aliyefariki dunia Oktoba 27 mwaka huu wakati akitekeleza jukumu la kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Marehemu Luteni Mlima alizikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam saa 10 alasiri
ambapo kabla ya hapo mwili wake ulipelekwa kwenye msikiti wa Maamur
ukitokea nyumbani kwake Mbezi Beach na kisha kuswaliwa kabla ya
kufikishwa kwenye makazi hayo ya milele.
Shughuli
za maziko zilianza kwa waumini walioongozwa na Imamu wa msikiti wa
Maamur, Ayoub Ali kuuweka mwili wa marehemu kwenye kaburi na kufuatiwa
na dua na baadaye kuzikwa kwa mujibu wa utaratibu wa JWTZ kwa kupigiwa
risasi baridi 4 hewani.
Akizungumza
wasifu wa marehemu, Meja Leonidas Benedict Luangisa alisema kuwa
marehemu alifariki dunia Oktoba 27 mwaka huu baada ya kupigwa risasi na
waasi wa M23 eneo la Kiwanja mlima Gavana akilinda amani nchini DRC.
Naye
Balozi Saleh Tambwe ambaye alitoa shukrani kwa kufanikisha mazishi ya
jemadari huyo wa JWTZ alieleza kufarijika kutokana na Jeshi la DRC
kutangaza kuukomboa mji wa Kiwanja ambao ndipo alipouawa marehemu Luteni
Mlima.
Pamoja
na Waziri Nahodha mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki Balozi Juma Mwapachu.
Kwa
mujibu wa Meja Luangisa marehemu Luteni Rajabu Ahmed Mlima alizaliwa
tarehe 30 Agosti mwaka 1977 katika Kata ya Gongoni wilaya ya Taboro
Mjini mkoani Tabora na kupata elimu ya Msingi katika shule ya msingi
Mahenge.
Meja
Luangisa alisema kuwa kuwa marehemu alipata Stashahada ya Juu ya
Sayansi ya Kopmyuta katika Taasisi ya Usimamizi wa Fedha(IFM) mwka 2005
na kujiunga na Jeshi tarehe 7 Januari mwaka 2008, na baadae kutunukiwa
Kamisheni ya Jeshi hilo..
Alisema
kuwa katika utumishi wake Jeshini alifanikiwa kuhudhuria Kozi
mbalimbali ikiwemo ya masuala ya Kinyuklia, Biolojia, na Kemia mwaka
2010 ambapo kabla ya hapo alipandishwa cheo kuwa Luteni Januari 10 mwaka
2009.
Kwa
mujibu wa wasifu wake marehemu alifariki akiwa Kamanda wa Platuni
Ulinzi wa Amani nchini DRC mwaka na vikosi vingine vya JWTZ nchini na
kabla ya kifo chake marehemu alijaaliwa kupata mtoto mmoja.
Sote
ni Wa Mwenyezi Mungu na Hakika sote tutarejea kwake, Mungu ailaze Roho
ya Marehemu Luteni Rajabu Ahmed Mlima Mahali Pema Peponi, Amin.
NA FULL SHANGWE BLOG
NA FULL SHANGWE BLOG
0 comments:
Post a Comment