Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi
inayotokana na zao la mnazi toka kwa Waziri wa
Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa
Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka,
kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la
mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na
Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara
(shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za
kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo
linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Picha ya pamoja ya Rais
Jakaya Mrisho Kikwete wakati na Waziri wa Maendeleo
ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath
Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia
njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao
la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.Picha na
IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali imedhamiria kukabiliana na maradhi ya
mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la
mnyauko.
Aidha, Rais
Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na
tatizo la minazi kwa sababu watu wengi katika baadhi ya maeneo ambayo uchumi
wake unategemea zao la mnazi wanakabiliwa na hatari ya kweli kweli ya kuathirika
kwa maisha yao.
Rais
Kikwete ametoa uhakikisho huo jana, Jumamosi, Novemba 16, 2013, wakati
alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha
wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara na ujumbe wake mjini Colombo.
Waziri huyo aliandamana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti ya Minazi ya Sri
Lanka.
Rais
Kikwete yuko nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa
Jumuia ya Madola (CHOGM) unaomalizika leo, Jumapili, Novemba 17, 2013. Mkutano
huo wa siku tatu, ulianza juzi, Ijumaa, Novemba 15,
2013.
Mheshimiwa
Pushpakumara na ujumbe wake walikuwa wanamwelezea na kumkabidhi Rais Kikwete
Ripoti ya Magonjwa ya Minazi iliyoandaliwa na wataalam wa minazi wa Sri Lanka
ambao walitembelea Tanzania Julai mwaka huu.
Wataalam
hao walitembea Tanzania na kufanya utafiti kuhusu ugonjwa unaolikabili zao la
minazi kufuatia ahadi ya Rais Mahinda Rajapaksa aliyoitoa kwa Rais Kikwete
wakati alipofanya ziara rasmi ya Tanzania Juni 27, 2013, na baadaye kushiriki
katika Mkutano wa Smart Partnership Juni mwaka
huu.
Rais
Rajapaksa alitoa ahadi hiyo baada ya kuelezwa na Rais Kikwete kuhusu zao la
kukauka kwa minazi nchini. Mnazi ni zao muhimu sana katika uchumi wa Sri Lanka
na ni zao tegemeo kwa wananchi wa Taifa-Kisiwa hilo kilichoko kusini mashariki
mwa India katika Barahri ya Hindi.
Wataalamu
waliofuatana na Waziri huyo wamemwambia Rais Kikwete kuwa ugonjwa unaolikabili
zao hilo la minazi ambao pia unashambulia minazi katika eneo la Caribbean hauna
tiba kwa sababu mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya utafiti imegundua dawa
hiyo.
Wataalam
hao ambao walikaa Tanzania kwa wiki moja, zikiwamo siku mbili katika Zanzibar,
wanasema kuwa zao hilo la mnazi, kama ilivyo katika nchi nyingine zinazolima zao
hilo, lina uwezo mkubwa wa kusaidia uchumi kupitia viwanda vidogo
vidogo.
Wakati
wakiwa Tanzania, wataalam hao wa Sri Lanka walifanya uchunguzi na utafiti kwa
karibu na wataalam wa Taasisi ya Utafiti ya Kilimo ya Mikocheni
(MARI).
0 comments:
Post a Comment