Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika,
wakati wakiwasili kwenye ukumbi wa Mkutano wa Tatu wa nchi za Kiarabu 'Afro
Arab', uliofanyika nchini Kuwait, leo Nov 19,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihudhuria mkutano mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro Arab' uliofanyika leo Nov 19,
2013, nchini Kuwait.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal,akihudhuria mkutano mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro
Arab' uliofanyika leo Nov 19,2013
akihudhuria mkutano mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro Arab' uliofanyika leo Nov 19,
2013, nchini Kuwait.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, (wa sita mstari wa tatu nyuma) akiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika wakati alipohudhuria katika
Mkutano wa mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro Arab' uliofanyika leo Nov 19,
2013 nchini KUwait. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
------
Makamu wa Rais wa
Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania
katika mkutano wa mashirikiano baina ya nchi za Afrika na zile za Kiarabu,
mkutano wa siku mbili unaofanyika katika nchini Kuwait. Mkutano huo
unaohudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 70 unalenga kuimarisha ushirikiano wa
Afrika na nchi za Kiarabu na unapitia makubaliano ya mkutano wa Sirte, Libya
uliofanyika mwaka 2011.
Mkutano huu unafanyika
kukiwa na mabadiliko kadhaa ya kiasiasa, kiuchumi na kimkakati baina ya nchi za
kanda hizi mbili huku taswira ya kukua kwa ushikiano huu zikionekana bayana kuwa
muhimu zaidi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Hii inatokana na nchi za kanda
hizi mbili, kukabiliwa na changamoto nyingi zinazofanana na zinazohitaji majibu
ya pamoja baina ya nchi za kanda hizi mbili. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja
na; mtikisiko wa uchumi, hali ya ulinzi na usalama, majanga yanayoikabili dunia,
usalama wa chakula na ugaidi.
“Changamoto hizi
hatuwezi kuzikabili wenyewe kama Tanzania ama kama Afrika. Tunahitaji wenzetu wa
ukanda huu wa nchi za Kiarabu kushirikiana nasi. Katika umoja wetu tutafanikiwa
kirahisi kuliko kama tutazikabili changamoto hizi tukiwa tumejitenga,” alisema
Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Tanzania licha ya kuwa
na wananchi wake katika nchi mbalimbali za dunia, tawimu zinaonesha kuwa, idadi
kubwa ya wananchi hao wapo katika nchi za Kiarabu hali inayoashiria umuhimu wa
kukuza mahusiano baina ya Tanzania pekee dhidi ya ukanda wa nchi za Kiarabu.
Katika siku za hivi karibuni kupitia Diplomasia ya Uchumi, Tanzania imefungua
njia kwa wawekezaji wa nchi za Kuwait, Oman na UAE na sasa taswira ya mahusiano
ya Tanzania na nchi hizi ni ya kuvutia ambapo inatoa fursa za kunufaika kiuchumi
kwa Tanzania kutoka katika ukanda huu kuliko kwa wadau wa maendeleo wa kanda
zingine ambazo Tanzania imekuwa ikishirikiana
nazo.
Akizungumza wakati wa
kutoa taarifa ya kikao hiki kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia yupo katika msafara wa Mheshimiwa Makamu wa
Rais, Bernard Membe alisema, kazi kubwa ya mahusiano baina ya Tanzania na nchi
za ukanda huu imejengwa na Rais Jakaya Kikwete na sasa milango imefunguliwa kwa
Watanzania kuchangamkia fursa za maendeleo hasa katika suala zima la masoko ya
bidhaa za kilimo, ufiugaji na utalii.
Katika Hotuba yake
kwenye mkutano huu, Mheshimiwa Makamu wa Rais licha ya kutoa shukrani na salamu
za Tanzania kwa Amiri wa Kuwait, Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah na
wananchi wa Kuwait na kwa viongozi wote wan chi za kanda hizi mbili, Mheshimiwa
Makamu wa Rais alifafanua kuwa Tanzania inatambua mahusiano ya kitamaduni,
kihistoria na kijiografia yaliyopo baina ya kanda hizi mbili na kwamba zaidi ya
theluthi mbili ya watu wa ukanda wa nchi za Kiarabu wanaishi Afrika hali
inayochagiza umuhimu wa uhusiano wa kanda hizi.
Pia Mheshimiwa Makamu
wa Rais alifafanua kuwa, Mkutanouliofanyika Libya mwaka 2011, haukuonesha
mafanikio ya wazi hasa katika miradi ya Maendeleo na akauomba mkutano huu wa
Kuwait, kuhakikisha kanda hizi zinaongeza spidi ya kufanikisha malengo ya
kimaendeleo, ili wananchi wa kanda hizi wazidi kunufaika kutokana na mahusiano
haya
Katika msafara huo,
Mheshimiwa Makamu wa Rais pia ameambatana na Waziri wa Kilimo na Chakula,
Enginia Christopher Chiza, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati wa SMZ,
Ramadhan Shaaban, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu, Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha, Servacius Likwelile na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Uledi Mussa. Pia katika msafara huo wapo wabunge Hamad Rashid na
Khalifa Khalifa.
Imetolewa
na:
Boniphace
Makene
Mwandishi wa Habari
wa Makamu wa Rais
0 comments:
Post a Comment