SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 15, 2013

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameitupia lawama Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA)

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe 
---
 Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameitupia lawama Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwa kile alichokieleza kulala kwao siku za mapumuziko na sikukuu kunarudisha nyuma ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Mwakyembe aliyasema hayo jana wakati wa ziara ya kikazi bandarini hapo akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Omari Issa.
Mwakyembe alisema watendaji na viongozi wa bandari, wamekuwa wakifanya kazi saa 24 ili kuhakikisha meli zinashusha mizigo haraka na wahusika wanachukua mizigo hiyo pasipo vikwazo.
“Bandari wanafanya kazi saa 24 kwa siku saba za wiki bila kupumzika, lakini wenzetu wa TRA wao sikukuu na siku za mwisho wa juma wanalala hali hii inaturudisha nyuma kimapato,” alisema Dk Mwakyembe.
Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.........

0 comments:

Post a Comment