Mtoto wa muigizaji mkongwe nchini, Mzee Small, Wangamba Mahmud Said Wangamba ameiomba serikali na makampuni aliyoyafanyia kazi baba yake kumsaidia gharama za matibabu ya baba yake yaliyosimama kwa sasa kutokana familia hiyo kushindwa kumudu.
Akizungumza na mtandao wa filamucentral, Mahmud alisema familia imeshindwa kuendeleza matibabu ya Mzee Small kwa muda mrefu kutokana familia hiyo kuwa na kipato kidogo na kushindwa kumudu gharama za matibabu na hivyo kuiomba serikali na makampuni aliyowahi kufanyanayo kazi yaweze kumsaidia.
“Sisi kama familia tunajisikia vibaya sana tunaposhindwa kumsaidia baba kwa sababu yeye ni kila kitu, mimi nasoma sina kipato, mzee toka mwaka jana mwezi wa tano mwaka jana alipomaliza dawa zake hajatumia dawa hadi leo kwa sababu hatuna fedha,”
“Lakini jambo linalotuuma hakuna hata kampuni ambayo imeonyesha kumsaidia kama Bakhresa alikuwa kuwa akifanya nao kazi hakuna msaada lakini pia Serikali kupitia menejimenti utumishi wa umma walikuwa wanafanya nao kazi wamemtosa yupo tu, pengine wanasubiri afe ndio waje kumzika,”anasema Mahmud.
Mzee Small anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ikiwa sambamba na kupoteza kumbukumbu anahitajka zaidi ya milioni moja na nusu kwa ajili ya matibabu kutokana na ushauri wa daktari kwani inasemekana kichwani kuna tatizo ambalo linamsababishia kupoteza kumbukumbu anahitaji dawa kwa ajili ya tatizo hilo na muda wa kupomzika.
Kwa anayeguswa na tatizo hilo anaweza kuitumia familia yake mchango wa matibabu kwa namba TIGO – PESA 0714 344 039 kumsaidia mzee Small.
Source: Filamu Central
0 comments:
Post a Comment