Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, akimlaki Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada
ya mgeni huyo kuwasili mchana huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo. Chama Cha
Kikomunisti cha China (CPC) ambacho ni rafiki mkubwa wa CCM kimealikwa
kutokana na kuwa Chama kilichosaidia sana harakati za ukombozi huo wa
nchi za kusini mwa Afrika. Katikati ni Balozi wa China hapa nchini, Lu
Youqing.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose
Migiro, akimlaki Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti
cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada ya mgeni huyo kuwasili mchana
huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili
ya kuhudhuria mkutano huo. Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho
ni rafiki mkubwa wa CCM kimealikwa kutokana na kuwa Chama kilichosaidia
sana harakati za ukombozi huo wa nchi za kusini mwa Afrika. Kushoto ni
Balozi wa China hapa nchini, Lu Youqing.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose
Migiro, akiwa na mgeni wakei Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti
cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada ya mgeni huyo kuwasili mchana
huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili
ya kuhudhuria mkutano huo. Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho
ni rafiki mkubwa wa CCM kimealikwa kutokana na kuwa Chama kilichosaidia
sana harakati za ukombozi huo wa nchi za kusini mwa Afrika.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose
Migiro, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti
cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada ya mgeni huyo kuwasili mchana
huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili
ya kuhudhuria mkutano huo. Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho
ni rafiki mkubwa wa CCM kimealikwa kutokana na kuwa Chama kilichosaidia
sana harakati za ukombozi huo wa nchi za kusini mwa Afrika.
"PANDA GARI HILI" Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose
Migiro, akimwelekeza kupanda gari Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti
cha Jamhuri ya watu ya China Ai Ping baada ya mgeni huyo kuwasili mchana
huu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili
ya kuhudhuria mkutano huo. Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) ambacho
ni rafiki mkubwa wa CCM kimealikwa kutokana na kuwa Chama kilichosaidia
sana harakati za ukombozi huo wa nchi za kusini mwa Afrika.
Msafara wa Ai Ping ukiondoka Uwanja wa Ndege. Imetayarishwa na Bashir Nkromo
---
Leo Jumatatu tarehe 07/10/2013 Chama cha Mapinduzi
kinapokea ugeni mkubwa wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini
mwa Afrika. Makatibu Wakuu hawa wanakuja kuhudhuria Mkutano wa Sita
ambao ni mwendelezo wa mikutano ya aina hii inayofanyika mara mbili
kwa mwaka.
Vyama vyote vya Ukombozi vitahudhuria Mkutano huu
utakaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 09 Oktoba. Vyama
hivyo ni ANC cha Afrika ya Kusini; FRELIMO cha Msumbiji, MPLA cha Angola;
SWAPO cha Namibia; ZANU-PF cha Zimbabwe na Chama mwenyeji CCM.
Mkutano wa Makatibu Wakuu utatanguliwa na mikutano
ya Jumuiya za Vijana, Wanawake na Maveterani itakayofanyika Jumanne
Oktoba 8, 2013.
Mkutano wa Sita wa Makatibu Wakuu utahudhuriwa pia
na ujumbe kutoka Chama rafiki cha Kikomunisti cha China utakaoongozwa
na Ndugu Ai Ping, ambaye ni Naibu Waziri anayeshughulikia Idara ya Kimataifa
ya Chama hicho.
Pamoja na mambo mengine Mkutano huu wa Sita wa Makatibu
Wakuu wa vyama vya Ukombozi kusini mwa Afrika utajadili utekelezaji
wa maazimio yaliyopitishwa katika kikao chao cha tano kilichofanyika
huko Tshwane, Afrika ya Kusini mwezi Machi, 2013.
Mojawapo ya maazimio hayo ni ujenzi wa Chuo cha Pamoja
cha Vyama hivi vya Ukombozi utakaofanyika Ihemi, katika mkoa wa Iringa.
Makatibu Wakuu wanatarajiwa kuzuru eneo la Ihemi tarehe 08/10/2013 kama
sehemu ya maandalizi ya majadiliano ya Mkutano huo wa Sita.
Mkutano huu utafunguliwa rasmi na Ndugu
Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi tarehe 09/10/2013.
Imetolewa na :-
Asha-Rose Migiro
KATIBU WA SIASA NA UHUSIANO WA
KIMATAIFA
CHAMA CHA MAPINDUZI
07/10/2013
0 comments:
Post a Comment