Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wanafuzi wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi(VETA) , Lindi kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana mkoani Lindi.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi na wa pili Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila na kushoto wa kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro Hamidi.
Mwanafunzi wa wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi(VETA), Lindi akimwonesha Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (aliyevaa kitenge) jana kifaa cha kukata vyuma katika karakana ya uungaji vyuma.
Mwanafunzi wa wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Lindi akimwonesha Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (aliyevaa kitenge) jana kifaa cha ufundi wa magari katika karakana ya ufundi wa magari.
Mama Salma Kikwete , akipata maelekezo kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Edwin Nduguru(kushoto) jinsi deep stick inavyofanya kazi ya kupima kiwango cha oil kilichopo katika injini ya gari alipotembelea karakana ya ufundi wa magari wa chuo hicho jana. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi (kulia) , Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Nassoro Hamidi (kushoto).
Mama Salma Kikwete (aliyevaa kitenge ) akiongea jambo na Meneja wa British Gesi Tanzania ambao ndiyo wafadhili wa mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli, Kate Sullam (kushoto) jana kwenye Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi(VETA) , Lindi .Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana kwenye Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi(VETA) Lindi . Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi na Kushoto wa tatu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, kushoto ni Afisa Uhusiano wa chuo hicho Dora Tesha.
Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mradi wa mafunzo ya gesi na mafuta ya Petroli jana kwenye Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi(VETA) Lindi . Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila.
Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Lindi.
Picha na Anna Nkinda-Maelezo
Picha na Anna Nkinda-Maelezo
0 comments:
Post a Comment