SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 12, 2013

Bonnah Trust Fund yazinduliwa rasmi leo Jijini Dar

Muasisi wa Mfuko wa Elimu ya Bonnah Trust Fund,Bi. Bonnah Kaluwa ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kipawa,jijini Dar es Salaam akizungumza machache wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Kuhamasisha elimu ya Tanzania ili isonge mbele uitwao Bonnah Trust Fund,uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ya Uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Kuhamasisha elimu ya Tanzania ili isonge mbele uitwao Bonnah Trust Fund,Meya wa Ilala,Mh. Jerry Silaa akisisitiza jambo muda mfupi kabla ya kuzindua Mfuko huo,mapema leo asubuhi kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kutoka Kushoto ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga,Meneja wa Huduma kwa Jamii kutoka kampuni ya Tigo,Bi Woinde Shisael,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Mushi,Muasisi wa Mfuko wa Elimu ya Bonnah Trust Fund,Bi. Bonnah Kaluwa pamoja na Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo,Meya wa Ilala,Mh. Jerry Silaa wakifurahia jambo mara baada ya kufanyika kwa Uzinduzi Rasmi wa Mfuko wa Bonnah Trust Fund,mapema leo asubuhi kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma kwa Jamii kutoka kampuni ya Tigo,Bi. Woinde Shisael akizungumza.
Burudani ya Muziki

Dogo akionyesha umahiri wake wa kucheza na baiskeli ya gurudumu moja.
Mamodel wakipita jukwaani na mavazi ya Mwanamitindo Maarufu nchini,Bi. Asia Idarous a.k.a Mamaa wa Mitindo.
Asia Idarous a.k.a Mamaa wa Mitindo akisalimia wadau.
Wadau.

CHANZO: BOFYA HAPA 

0 comments:

Post a Comment