SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 12, 2013

WATOTO AGUSTINO NA REBEKA WATELEKEZWA NA WAZAZI WAO HUKO MBEYA.

 Agustino Steven (8) akiandaa ugali ale na dada yake.

 Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakichambua mboga aina ya mchicha 
 Mwenyekiti wa  Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
 Agustino Steven (8) akipika mchicha
 Hii ndiyo sahani yao wanayotumia kwa ajili ya chakula 
 Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) hapa wakila chakula walichopika wenyewe
 Unga pamoja na maharage
 Hili ndilo sanduku lao
 Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakiwa nje ya nyumba wanayoishi.
****
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi matano bila huduma za msingi.

Watoto hao wamefahamika kwa majina ya Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza  shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei mwaka huu ambapo Baba inasadikika alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako inasemekana ameoa mke mwingine.

Wamesema Mama yao alielekea Mbozi ambako pia naye inasadikika ameolewa na mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila kuwa na huduma za msingi kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa  Nyumba mtaa wa Jakaranda Airport.

Aidha watoto hao waligundulika baada ya kukutwa mitaani wakitafuta riziki kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha kupeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500  ambazo huzitumia kununua mahitaji ya nyumbani pamoja na kujipikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Amesema majirani pia waendelee kuwa karibu na watoto hao hadi pale wazazi wao watakapopatikana kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanaendelea na masomo kama kawaida.

Amesema kitendo kilichofanywa na wazazi hao ni cha kinyama hivyo wakipatikana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ambapo pia alitoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kikatili.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa www.mbeyayetu.blogspot.comumebaini kuwa Wazazi hao wanatabia kama hiyo kutokana na kuwahi kumtelekeza binti yao mwenye umri wa miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Salome Steven ambaye hakuwahi kupelekwa shule hivyo kuachiwa jukumu la kuwalea wadogo zake.

Kutokana na ugumu wa maisha binti huyo katika harakati za kutafuta chochote kwa ajili ya wadogo zake ameishia kuzalishwa mtoto wa kiume ambaye ana mwezi mmoja sasa na kuwakimbia wadogo zake nay eye kukimbilia kwa rafiki yake.

Pia Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia limeamua kulifuatilia suala hilo kwa kumtafuta kijana aliyemzalisha binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hezron ambaye imedaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti ).
CHANZO BOFYA HAPO CHINI:

0 comments:

Post a Comment