Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akiangalia moja kati eneo lililotawanywa solar panel za kuzalisha umeme.Picha na Chadema
****
Katibu Mkuu
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
,Chadema Dr Wilbroad Slaa Jumapili
13 Oktoba amesafiri kurudi Tanzania baada ya Ziara yake iliyomchukua wiki
tatu nchini Marekani. Dr Wilbroad Slaa aliwasili nchini Marekani tarehe 21 Septemba 2013 akiambatana na Mkewe
mama Josephine Mushumbuzi na kupokelewa na Uongozi wa Chadema DMV. Tarehe 22 Septemba 2013 Dr Slaa alifanya
mkutano uliojumuisha wanajumuia ya Watanzania waishio katika Majimbo ya
Washington, Maryland na Virginia.
Katika ziara
yake Dr Slaa alitembelea majimbo ya North Carolina na Alabama ambako
alitembelea Vyuo Vikuu na Taasisi mbalimbali na kujifunza Shughuli nyingi za
Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Afya, Nishati na Uchumi.
Akizungumza
akiwa uwanja wa Ndege wa Dulles mjini Washington Dr Slaa alisema alichojifunza
akiwa Marekani anatarajia kupeleka maarifa hayo Tanzania ili yaweze kumkomboa
Mtanzania kutoka katika Umaskini. Moja katika mambo ambayo amejifunza ni namna
ya kutumia nishati ya Jua kuzalisha umeme hasa kwa wakazi wa Vijijini.
0 comments:
Post a Comment