SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 7, 2013

Mama Kikwete akiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa ubongo cha Kuwait kushirikiana na Tanzania kutoa mafunzo kwa watoto hao.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za uchoraji zinazofanywa na watu wenye ulemavu wa ubongo wanaolelewa katika kituo Kharafi Kids Activity Center wakati Mama Salma alipotembelea kituoni hapo tarehe 6.5.2013.

Na Anna Nkinda – Kuwait

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa Ubongo kilichopo nchini Kuwait kushirikina na Tanzania ili waweze kufanya kazi kwa pamoja ya kuwasaidia na kutoa mafunzo kwa watoto wenye matatizo kama hayo waliopo nchini.

Mama Kikwete ametoa ombi hilo alipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kuona jinsi wanavyotoa mafunzo kwa watoto hao ambayo yameweza kuwabadilisha akili zao  na kuwa sawa na za watu wengine.


Amesema kuwa watoto wenye mtindio wa ubongo hata nchini wapo na wanapata mafunzo katika vituo vichache zilivyopo lakini kama watashirikiana kwa pamoja wataweza kubadilishana ujuzi ambao utawasaidia kutoa  mafunzo mazuri zaidi kwa watoto hao.

“Ninawapongeza kwa  kwa kazi kubwa na nzuri  mnayoifanya ya kutoa mafunzo kwa watoto hawa kwani  ni jambo jema  kuwasaidia watu wenye matatizo.

 Mama Kikwete amesema watoto hawa wakipewa mafunzo akili yao itakuwa sawa na watu wengine, wakiwa wakubwa na kufikia umri wa kujitegemea wataweza kufanya kazi mbalimbali za maendeleo ambazo zitawaingizia kipato na  kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Samira  Al-Saad amesema kuwa kama watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo watapelekwa  shule mapema zinazotoa mafunzo kwa ajili yao  watapona na kuwa na  akili sawa na watu wengine.

Dkt. Samira amesema kuwa wazazi wengi hawajui kwamba matatizo ya mtindio wa ubongo yanatibika kama mtoto akipewa elimu ya darasani na kufanyishwa mazoezi ambayo yatamsaidia kufanya  shughuli zake mwenyewe bila ya kutegemea msaada wa jamaa zao.

Dkt. Samira amesema kituo hicho kilifunguliwa mwaka 1994 na hadi sasa kina wanafunzi  120  ambao wanapata mafunzo ya nadharia na vitendo na kinajiendesha kwa kupata msaada kutoa Serikalini, watu na mashirika binafsi ya ndani na nje ya nchi.

Aliendelea kusema kuwa umri wa watoto wa kuanza masomo ni  miaka sita  hadi 15 na kama mwanafunzi atakuwa amevuka miaka 15 atajifunza zaidi mafunzo ya vitendo ambayo yatamuwezesha kujitegemea hapo baadaye.

Dkt. Samira amesema wanafunzi wetu wameweza kupata ajira sehemu mbalimbali hii ni baada ya kupata mafunzo ambayo yamewafanya kuwa na akili sawa na watu wengine ambao hawana matatizo haya, kuna baadhi yao tumewaajiri hapa na hivi  sasa wanawafundisha wanafunzi wenzao.

Mama Kikwete pia alitembelea Kituo cha Al-Kharafi ambacho kinatoa huduma ya mazoezi kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubungo  na kuona jinsi watoto hao wanavyofanya mazoezi yao.

Kituo hicho kinapokea  watoto wenye umri wa kuanzia miaka minne hadi  12 ambao wanafanya mazoezi kwa kucheza michezo mbalimbali ambayo inawabadilisha akili zao na kuwa katika hali ya kawaida .

Akiwa katika kituo hicho alijionea kazi mbalimbali zinazofanywa na watoto hao ambazo ni uchoraji, ushonaji, upishi  pia aliona michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyimbo na maonyesho ya mavazi.

0 comments:

Post a Comment