SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.
Showing posts with label Mama Kikwete akiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa ubongo cha Kuwait kushirikiana na Tanzania kutoa mafunzo kwa watoto hao.. Show all posts
Showing posts with label Mama Kikwete akiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa ubongo cha Kuwait kushirikiana na Tanzania kutoa mafunzo kwa watoto hao.. Show all posts

Tuesday, May 7, 2013

Mama Kikwete akiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa ubongo cha Kuwait kushirikiana na Tanzania kutoa mafunzo kwa watoto hao.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za uchoraji zinazofanywa na watu wenye ulemavu wa ubongo wanaolelewa katika kituo Kharafi Kids Activity Center wakati Mama Salma alipotembelea kituoni hapo tarehe 6.5.2013.

Na Anna Nkinda – Kuwait

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa Ubongo kilichopo nchini Kuwait kushirikina na Tanzania ili waweze kufanya kazi kwa pamoja ya kuwasaidia na kutoa mafunzo kwa watoto wenye matatizo kama hayo waliopo nchini.

Mama Kikwete ametoa ombi hilo alipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kuona jinsi wanavyotoa mafunzo kwa watoto hao ambayo yameweza kuwabadilisha akili zao  na kuwa sawa na za watu wengine.