SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 7, 2013

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU KWA SHULE ZA SEKONDARI TANGA.


 Meneja Mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway akikabidhi baadhi ya vitabu vya sekondari kwa afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa  ikiwa ni msaada ulitolewa kuchangia elimu  toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila, anaeshuhudia wakwanza kulia ni  Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga
Kulia ni Afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa ikimkabidhi kati ya vitabu vilivyotolewa kwa lengo la kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Mwishoni mwa wiki Airtel ilitoa vitabu kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu,  Kwendimu na Magila,. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga.

*********

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa  itabu vya hesabu,chemistry na baologia vyenye thamani ya shilingi milioni 12 kwa shule nne za mkoa wa Tanga.  

Msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  wa kusaidia ukuaji wa sekta ya limu kupitia kampeni yake ya shule
yetu.

Akipokea vitabu hvyo kwa niaba ya shule za mkoa wa tanga afisa elimu
wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa alisema,“ tunawashukuru Airtel kwa msaada huu wa vitabu kwani utasaidia kupunguza tatizo lauhaba wa  vitabu kwa shule zilizopatiwa msaada huo na kuongeza kiasi cha ufaulu kwa wanafunzi. Tunaomba juhudi hizi zisihishie hapaziendelea katika shule mbalimbali mkoani hapa na mikoa mingine yaTanzania ili kuondoa ujinga na umaskini na kuwapa watoto wetu elimu bora kwani hawa ndio taifa la kesho.

Kwa upande wake meneja mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na  Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni yake wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini. Chini ya mpango maalumu wa Shule yetu tumeweza kuzifikia shule nyingi za sekondari nchini.

Akiongea kwa niaba za shule zilizopokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule ya secondari ya Mkuzi juu Bwn Victor Mwenda alisema”  Tunatoa shukurani kwa Airtel kwa msaada wa vitabu katika shule zetu zasekondari, kwa hatua hii itasaidia kupunguza tatizo la vitabu linalozikabili na kuongeza ufanisi katika masomo ya sayansi. Tunawaomba wanafunzi wavitunze na kuvitumia vizuri hivi vitabu kwani
ni nyenzo muhimu katika elimu ya sekondari.

Vilevile Meneja wa huduma za jamii wa Airtel Tanzania Bi Hawa Bayuni alidokeza kuwa Airtel iko katika mkakati wa kuanza awamu nyingine ya ugawaji wa vitabu kwa shule za sekondari kwenye kila mkoa ikiwa ni program yake ya mwaka huu ya kurudisha kwa jamii kupitia elimu “tunaingia katika awamu ya mpya ya utowaji wa vitabu kwa shule ngingi zaidi  kila mkoa hapa Tanzania, mradi wetu huu utazingatia zaidi shule za sekondari zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu kwamba ni shule zipi zina uhitaji  mkubwa wa vitabu na kushauri  ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule yetu” alieleza Bayumi.
CHANZO: BOFYA
  
Airtel toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka nane iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1500 za sekondari zilizopo Tanzania kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa  yote  na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania na pia kukarabati miundombinu ya shule kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni hatua ya Airtel kukuza kiwango cha elimu kwenye maeneo mbalimbali Tanzania aliongeza Bayumi.

Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi mkoa ni Tanga ni pamoja na shule ya sekondari ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila.mkakati ni kuendelea kutoa vitabu kwa shule mbalimbali nchini ambapo droo ya shule za sekondari zitakazo faidika na vitabu kwa mwaka huu wa 2013 -2014 itafanyika mwenzi Juni  na kutoa nafasi kwa shule nyingine nyingi za sekondari nazo kufaidika na mpango huu wa Airtel shule yetu.

0 comments:

Post a Comment