Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA)Picha juu amekamatwa na polisi jana hii kwa tuhuma kuwa ndiye chanzo cha kuhamasisha wafanya biashara
wadogo wadogo (wamachinga) kufanya vurugu huko Iringa.Askari
polisi wa kutuliza ghasia (FFU) katika Manispaa ya mji wa Iringa pia
imewakamata zaidi ya watu hamsini, akiwemoo aliyekuwa mgombea udiwani
katika kata ya Mvinjini, Abuu Majeck.
Biashara zilisimama wakati wa sekeseke hilo, moshi ulitanda kutokana na matairi kuchomwa moto katika barabara za kuu ya Iringa-Dodoma na ile ya Mashine Tatu. Jana hii pia, Mbunge huyo alikuwa katika eneo la chuo cha Tumaini kwenye harambee iliyokuwa imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kama inavyoonekana kwenye pichaa chini

Mbunge wa iringa Mjini-Chadema Mchn Msigwa (kulia)akizungumza na msaidizi wa askofu wa KKKT dayosisi ya Iringa muda mfupi kabla ya kukamatwa na polisi jana




0 comments:
Post a Comment