SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 30, 2012

Vodacom Foundation yatoa Milioni 20 kuweza watoto yatima.

 Meneja wa huduma za jamii wa Vodacom Foundation Mwamvua Mlangwa,  akikabidhi mfano wa hundi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni 20, kwa Mkurugenzi wa kituo cha Tanzania Mitindo House, Khadija Mwanamboka, Kwa ajili ya kuanzisha chuo cha mafunzo ya Mitindo kwa Watoto yatima.
****
Dar es Salaam, Zaidi ya watoto yatima 50 waishio katika mazingira magumu watapata mafunzo ya ubunifu wa mavazi. Hii inafuatia kuanzikwa kwa kwa kituo cha ubunifu wa mavazi ,  (Mitindo House) kitakachokuwa chini ya Mwanamitindo maarufu, Hadija Mwanamboka.
Kituo hicho kitatoa mafunzo ya ushonaji, ubunifu wa mavazi, na utengenezaji wa vito mbalimbali kimefadhiliwa na mfuko wa huduma za jamii wa Vodacom (Vodacom Foundation)
Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi ya shilingi Milioni Ishirini, Mkurugenzi wa kituo hicho, Hadija Mwanamboka, amesema kuwa lengo lao ni kuwawezesha watoto yatima waishio katika mazingira magumu na wasio na elimu kuweza kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe kutokana na ujuzi watakao upata.
“Tutatoa mafunzo kwa watoto wanaoishi katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima, yatakayo wawezesha kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika majukwaa ya sanaa na baadae kuwawezesha kujiajiri wao wenywe.”
“Mafunzo haya yatatolewa kwa mwaka mzima, wanafunzi ishirini na tano watapata mafunzo ya ushonaji na ubunifu wa mavazi na wengine 25 watapata mafuzno ya uchongaji wa vito mbalimbali na uchoraji,” alisema Hadija.
Kwa upande wake, Meneja wa Huduma za jamii wa Vodacom Foundation,  Mwamvua Mlangwa amesema kuwa Vodacom Foundation imedhamiria kuboresha maisha ya jamii ya watanzania wanaoishi katika mazingira magumu.
“Vodacom Foundation itaendelea kuwaunga mkono watanzania hususani wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kujenga maisha yao na kusaidia kukua kwa uchumi wa nchi kupitia mipango mbalimbali tuliyonayo katika kitengo chetu,” alisema Mlangwa.
Kuhusu Vodacom Tanzania:
Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na  jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation.   Vodacom Foundation  ina nguzo kuu tatu: Afya,  Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi  sasa taasisi hiyo  imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha,  imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa  na kampuni mama ya Vodafone  . 
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia  teknolojia ya kisasa  ya  mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki  hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na  asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa  Super Brand (Chapa Bora Zaidi)  kwa miaka  mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment