SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 30, 2012

Taswira Kutoka Tuzo za Beffta 2012

Fashionista Mamaa Jestina George aka mama Iman ndani ya mambo ya Red Carpet
Catwalk Professor akila pozi baada ya kushinda tuzo yake ya Beffta
Fabrice Muamba akiwa na furaha tele baada ya kukaribishwa kwa shangwe na shauku na wadau
kutoka Kulia Ceo wa Beffta Pauline Long akitaja washindi wa tuzo za mwaka 2012
Msanii Nathan baada ya kumkabidhi tuzo mama yake
Mtangazaji Nguli wa zamani wa ITV sir Trevor McDonald akisema machache baada ya kupokea Tuzo ya Beffta ''LIFE TIME ACHIEVEMENT ''
show zikiendela
Makamuzi yakiendelea
Frank Eyembe akila pozi na Fabrice Muamba
Frank akiwa na Actor Wale Ojo baada ya kunyakua tuzo ya best actor
kutoka kulia Mshindi wa best of Best Fashion Choreographer 2012 Yvonne, Jestina, Peace na Frank 
kutoka kulia Mshindi wa best of Best Fashion Choreographer 2012 Yvonne, Jestina, Peace na Frank 
sehemu ya kadamnasi ilivyofurika wadau kutoka sehemu mbalimbali
Warembo waking'ara ndani ya red Carpet

****
Salaam,

Urban Pulse na Miss Jestina blog wanakuleta taswira mbalimbali kutoka katika tuzo za Nne Beffta 2012 zilizofanyika jumamosi tarehe 27 Octoba 2012 ndani ya Ukumbi wa HIPPODROME,GOLDERS GREEN, LONDON NW1 7RP. Tuzo hizi ziliandaliwa maalum kwa ajili ya kutambua michango mbalimbali ya wasanii na wataalam katika tasnia ya luninga, Filamu, Internet, Mitindo, Magazeti, Majarida, Muziki,Tamthilia,Tovuti na Blogs, Kucheza, Mashairi, na michango ya watu fulani  mashuhuri katika kukuza au kuimarisha  jamii ya watu weusi hususani wafrika waishio hapa nchini Uingereza.

Mojawapo ya tuzo za muhimu Beffta zilikwenda kwa mtangazaji nguli wa zamani wa  ITV Sir Trevor Mcdonald aliejinyakulia tuzo ya " Life time Achievement" kutokana na mchango wake katika tasnia ya utangazaji.

Mbali na hapo tuzo za Beffta zilienda maili zaidi kwa kumkaribisha mchezaji wa zamani kutoka timu ya  Bolton ambaye alifariki uwanjani kwa mda wa dakika 54, lakini kutokana na nguvu pamoja na miujiza ya mwenyezi mungu kwa kuwawezesha  madaktari aliweza kufufuka na kuwa hai hadi leo hii. Mchezaji huyu mwenye asili ya Kikongo aitwaye Fabrice Muamba alifunga pingu za maisha hivi karibuni na mchumba wake Shauna Magunda pia ndio  aliekua mgeni rasmi katika sherehe hizi za tuzo za Beffta 2012.

Tuzo za Beffta zimeanzishwa miaka minne iliyopita na Pauline Long kutoka Kenya ambaye ndio CEO wa tuzo za Beffta.

Asanteni,

Urban Pulse wakishirikiana na Miss Jestina Blog

0 comments:

Post a Comment