Mmoja wa Maofisa wa Polisi akielekeza jambo kwa Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga (tatu shoto) ,ACP Kilonzo kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi (mwenye miwani) pamoja na ASP Msuyale ( wa tatu mstari wa nyuma) wote kutoka nchini Tanzania, kuhusiana na mambo ya usalama barabarani.
Maofisa hao wakuu waandamizi wa jeshi la polisi kutoka nchini Tanzania walikuwa nchini Ujerumani kwa ziara ya mafunzo ya wiki moja (21/10 - 27/10/20120),katika jimbo la Lower Saxon,ambapo pia walitembelea Mji mkuu wa jimbo hilo Hannover, Neunberg, na Gottingen.
Mmoja wa Maofisa wa Polisi (mwenyeji) akiwaelekeza jambo kwa Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) namna ya matumizi mbalimbali ya usalama barabarani.
Aidha ziara hiyo ilihusisha mambo mbalimbali ya usalama barabarani ikiwemo kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha, na rader ya kawaida, ukaguzi wa malori ya mizigo na mambo mengine mengi..
Mmoja wa Maofisa wa Polisi akimuelekeza Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga namna ya kuangalia upimaji mwendo kasi kwa kutumia mtambo maalum unaopiga picha kuhusiana na uendeshaji magari barabarani.
Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale wakielekezwa namna ya leseni za madereva zinavyokuwa.
Maofisa wa juu wa kutoka jeshi la polisi nchini Tanzania, Kamanda Wa Kikosi cha Usalama Barabarani,SACP Mohamed Mpinga,ACP Kilonzo pamoja na ASP Msuyale (wote watatu pichani kati) wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao.Picha zote kwa hisani ya SACP Mohammed Mpinga - CO Traffic.
0 comments:
Post a Comment