MKURUGENZI Kanda ya Afrika na Ulaya wa Taasisi ya Project Hope ya Marekani, Katerina Takovska (kulia) akimkabidhi msaada wa vifaa vya hospital pamoja na madawa vyenye thamani ya dola milioni moja ($1.1ml) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Dk.Sira Ubwa Mamboya makabidhiano hayo yalifanyika katika bohari kuu la Madawa Mnazimmoja mjini Zanzibar.
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Saleh Mohammed Jidawi (katikati) akiangalia tarehe ya kumaliza muda msaada wa madawa waliopewa na Taasisi ya Project Hope ya Marekani kulia Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Dk.Sira Ubwa Mamboya na msaidizi mkurugenzi kanda ya Afrika na ulaya, mshauri mwandamizi wa masuala ya Afya , Dalibor Tasevski wakiwa katika bohari kuu la madawa mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Dk.Sira Ubwa Mamboya akitoa salaam za shukrani muda mfupi baada ya kupokea misaada hiyo
CHANZO NA HAKI NGOWI.
0 comments:
Post a Comment