Mkuu wa Polisi Jamii wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Issaya Doya akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa VodacomTanzania Mwamvita Makamba, wakati wa sherehe ya kakabidhi rasmi kituo hicho kilichakarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation kwa thamani ya shilingi Milioni 17,tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Thobiasi Andengenye akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wakati wa hafla ya kukabidhiwa kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha , kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Tanzania kwa thamani ya Shilingi Milioni 17 tangia kijengwe mwaka 1967.katikati ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu ( OCD ) Mathias Nyange.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha Polisi Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967,kwa gharama ya shilingi milioni 17.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya kaskazin Nguvu Kamando.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Jumla ya shilingi Milioni 17 zilitumika katika kukarabati kituo hiuchi. Kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini.Nguvu Kamando.
Mkuu wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Arusha.(INSP)Amilton Matangi akiwaonyesha moja ya chumba cha mahabusu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kulia na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho,Jumla ya shilingi Milioni 17 zilitumika kukikarabati kituo hicho tangia kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kushoto akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando kulia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba akishuhudia, Jumla ya shilingi Milioni17.zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC).Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 17, wakishuhudia ni Mkuu wa Kituo hicho INSP Amilton Matagi ,Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba ,Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Nguvu Kamando.
Hichi ni Kituo cha Polisi Cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kikionekana katika muonekano mpya baada ya kukarabatiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kiasi cha shilingi Milioni 17 kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.
Waandishi wa habari wakiwa kazini kama kawa wakati wa Makabidhiano rasmi ya Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation, tangu kujengwa kwake mwaka 1967,Maboresho hayo yamegharimu kiasi cha shilingi milioni 17.
0 comments:
Post a Comment