SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, January 31, 2012

BINTI YATIMA AKATISHWA MASOMO, AZALISHWA, ATELEKEZWA AZUNGUKA KUTAFUTA KAZI ZA NDANI

Mtoto yatima Hawa Saidi (19) mkazi wa kijiji cha Ulembo wilaya ya Njombe mkoani Iringa amejikuta akiishi maisha ya kuhangaika mitaani na mtoto wake wa mwaka mmoja na wiki moja baada ya kuzalishwa mtoto huyo na mfanyakazi mwenzake wa ndani na kufukuzwa kazi.
Binti huyo ambaye jana usiku alikutwa akizunguka katika mitaa ya Frelimo muungano katika manispaa ya Iringa anadai kuwa wazazi wake walifariki dunia akiwa darasa la kwanza na kulazimika kukatisha masomo yake na kwenda Dar es Salaam kusaka kazi kwa kipindi cha miaka miwili kwa mshahara wa shilingi 20,000 kwa kila mwezi sasa hana njia nyingine ya kuishi na hivyo kuomba wasamaria wema kumsaidia kurudi shule ama kupewa kazi ya ndani ili kuweza kusomesha mtoto wake na yeye mwenyewe kupata uhakika wa maisha.
Wadau binti huyo asubuhi hii ametinga nyumbani kwa mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ili kuomba kusaidiwa kutafuta wasamaria wema wa kumsaidia .
Hivyo kama upo tarayi kumsaidia waweza kuwasiliana na mmiliki wa mtandao huu (http://francisgodwin.blogspot.in/) kwa namba +255754 026299/+255712750199 ili kuweza kumsaidia kwa lolote binti huyo ,sikiliza Radio Country Fm 88.5 saa 30.30 asubuhi hii kujua zaidi.

0 comments:

Post a Comment