ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Wednesday, August 31, 2011

Waasi Libya Wakataa Jeshi La Amani La UN

Wananchi wa Libya wakisherehekea Eid mjini Tripoli
Uongozi wa mpito nchini Libya umekataa wazo la kuweka jeshi lolote la kimataifa aina yoyote ya jeshi la kimataifa, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya amesema.
Ian Martin amesema Umoja wa Mataifa ulifikiria kupeleka waangalizi wa kijeshi nchini humo.
Taarifa hizo zimekuja wakati wapiganaji wanaolitii Baraza la Mpito wakikaribia ngome ya Gaddafi ya Sirte kutokea mashariki na magharibi.
Wamepewa hadi Jumamosi kusalimu amri.
Hata hivyo msemaji wa Kanali Gaddafi aliyekimbia Moussa Ibrahim, amekataa amekataa kukubaliana na kusalimu amri, Shirika la habari la AP linaripoti.
"Hakuna taifa lenye heshma yake litakubali kutii makataa kutoka kwa genge lenye silaha," alisema kwa njia ya simu alipozungumza Jumatatu usiku na AP.
Bw Ibrahim alirejea ahadi ya Kanali Gaddafi ya kumtuma mwanawe Saadi kufanya majadiliano na waasi na kuunda serikali ya mpito, shirika hilo la habari limesema.
'La Libya ni maalum'
Mwakilishi msaidizi wa Libya katika Umoja wa Mataifa Ibrahim Dabbashi, ameiambia BBC kwamba hali ya Libya ilikuwa ya kipekee
"Umoja wa Mataifa unaangalia uwezekano wa kuweka wanajeshi wa kulinda amani nchini humo lakini mgogoro wa Libya ni suala maalum.
"Si vita vya wenyewe kwa wenye, si mzozo kati ya vyama, ni watu ndio wanaojilinda wenyewe dhidi ya udikteta."
Hata hivyo, Bw Martin alisema Umoja Wa Mataifa unatarajia kuombwa kusaidia kuimarisha jeshi la polisi"
Kwa sasa hatutarajii kuomba jeshi la kulinda amani," alisema baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
"Ni wazi kuwa walibya wanataka kuepuka aina yoyote ya jeshi kuletwa na Umoja wa Mataifa au yeyote," alisema.
Bw Martin aliongeza kuwa changamoto kubwa kwa Umoja wa Mataifa kuisaidia nchi kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia.

Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Swala Ya Iddi Msikiti Wa Kichangani,Magomeni Mapipa Daressalaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Iddi katika msikiti wa kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa Iddi baadhi ya waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Picha zote: Freddy Mar-IKULU

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Shein Ahudhuria Swala ya Idd el Fitri Bwawani Hotel Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akiwahutubia wananchi na waislamu katika baraza la Iddi el Fitri lililofanyika huko ukumbi wa Salama hall Bwawani Hotel mjini Zanzibar.
Makamo wa kwanza wa Rais Seif Sharif Hamadi akisalimiana na Waziri wa katiba na Sheria wa Zanzibar Abubakari Khamis Bakari baada ya kuingia katika kiwanja cha maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
Rais wa Zanzibar Alhaji Dr,Ali Mohd Shein pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali na wananchi,wakiwa katika swala ya iddi ambayo imeswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
Baadhi ya kinamama waliohudhuria katika swala ya Idi Elfitri huko katika kiwanja cha Maisara mjini Zanzibar
 Wananchi mbalimbali wa Zanzibar wakisikiliza hotuba ya Idi Elfitri baada ya kumaliza kuswali swala ya Idi huko katika kiwanja cha maisara zanzibar.
(Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu -Zanzibar).

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI SWALA YA EID EL FITR MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agosti 31.
Immam Mkuu wa Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Masoud Mohamed Jongo,  akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid El-Fitr iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo, Agosti 31, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agosti 31
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Agoost 31.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El- Fitr, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo Agost, 31
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El-Fitr leo, Agosti 31.
(Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais).

Tuesday, August 30, 2011

EID MUBARAK TO ALL MUSLIM ALL OVER THE WORLD

Happy Eid

On behalf of 24 SEVEN 365 i would like to take this opportunity to wish you all a very Happy & Peaceful Eid. May allah accept your good deeds forgive your transgression & case the sufferings of all peoples around the Globe.
Happy Eid Mubarak.

Monday, August 29, 2011

Naibu Balozi Wa Tanzania Nchini Uingereza Ashiriki Kwenye Futari Iliyoandaliwa na Reading Eastern African Community


Mtoto mwanajumia nae akila futari
Mh Naibu Balozi(wa pili kulia) akipata futari
Futari ilienda sambamba na kubadilishana mawazo
Baadhi ya viongozi wa REACO wakipata Futari
Mh Chabaka akifurahia jambo wakati Afisa wa UBalozi Kiondo akiteta na Ustaadhi Sungura .
Mh Naibu Balozi Chabaka akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa REACO
Picha ya pamoja na wanajumuia
Baadhi ya Viongozi wa REACO katika Picha ya pamoja
-----
Salam Alleykum,


READING EASTERN AFRICAN COMMUNITY(REACO) Iliandaa futari maalum leo jioni 28.8.11 na kuwaalika wanajumuia mbalimbali kutoka  Reading, London, Coventry na sehemu nyingine ili kupata futari kwa pamoja. Hii ni desturi ambayo hufanyika kila mwaka wakati huu wa mwezi mtukufu ramadhani. Lengu kuu haswa ni kujumuika pamoja katika kudumisha upendo, amani na umoja kwa wana jumuia pamoja,kuzingatia yale yote yalio mema na kukataza yalio Mabaya.

Mgeni Rasmi wa siku ya leo alikuwa Mh Naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na baadhi ya maofisa wa ubalozi wetu wa Tanzania Hapa London.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa REACO Said Mahmud tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioitikia mwito na kuja kujiunga nasi. Tunawashuru sana.

Kwa maelezo au mawasiliano zaidi tafadhali tutumie email ifuatayo, reaco@hotmail.co.uk

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE

Sunday, August 28, 2011

Anna Breaks Fast After 288 Hours, Nation Relieved

Anna Hazare ended his 12-day fast Sunday morning before tens of thousands of cheering supporters at Ramlila Maidan by sipping a glass of coconut water with honey offered to him by two girls.
The nation, particularly the government of Prime Minister Manmohan Singh, heaved a collective sigh of relief at the resolution of a major national crisis as the 74-year-old activist ended his fast at around 10.20 a.m. He began his fast Aug 16 morning and completed 288 hours of fasting. 

RAIS DK.JAKAYA KIKWETE NA MAKAMU DK. GHARIB BILAL WAFUTURU PAMOJA NA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Meck Dadick, wakiomba dua kwa pamoja baada ya kupata futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake Oysterbay jijini jana, Agosti 27
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad saul,  wakiwa pamoja wakati wakisubiri muda wa swala kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, baada ya hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika makazi yake oystebay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27. 
Rais Dkt. Jakaya kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiagana na baadhi ya wananchi waliofika katika futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa rais katika makazi yake Yosterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27, ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru kwa kuhudhulia hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya CXC Africa Ltd, Charles Hamkah, wakati alipowaalika wageni katika hafla ya futari katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu katika makazi yake Oysterbay Dar es Salaam jana Agosti 27.
(Picha Zote na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais)

Mama Salma Kikwete Aendesha Harambee Ya Kuchangisha Fedha Kwaajili Ya Tamasha La MOWE

Mwenyekiti wa Taasisi wa WAMA pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Wajasiriamali Aug 26,2011 jinini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) 2011 litalofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mwaka huu Taasisi ya WAMA ndio mratibu wa Tamasha hilo.Jumla ya zaidi milioni 55 zimechangwa katika hafla hiyo na kauli mbiu ya mwka huu ya MOWE ( MIAKA 50 WANAWAKE WAJASIRIAMALI TUNAWEZA-TUTUMIE FURSA),(kulia ni Mwenyekiti wa MOWE Tanzania Elihaika Mrema,na (kushoto) ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Consolata I.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Alexio Musindo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) yaani Month of Women Enterprenuers,
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa muwakililishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania Gloria Kavishe(kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa uchangiaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) August 26,2011, Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule ya mfano ya watoto yatima WAMANAKAYAMA iliopo Rufiji mkoa wa Pwani,
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mwakilishi wa Bank ya CRDB (kulia)kwaajili ya kuchangia tamasha la wajasiriamali wanawake (MOWE) 2011 , (aug 26,2011)) jijini Dar es Salaam, Zaidi ya shiligi 55 milioni zimechangwa.(55,368,500/)
Baadhi ya Wanawake wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Slama Kikwete (Aug 26,2011) katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya MOWE na vbaadhi ya viongozi wa meza kuu akiwepo Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.
(Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO)

Ikulu Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Uamuzi Wa Rais Jakaya Kikwete Juu Ya Swala La David Jairo

Tarehe 21 Julai, mwaka huu, 2011,Katibu Mkuu Kiongozi Bwana Phillemon Luhanjo, akitumia madaraka yake ya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Umma, alitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, ili kupisha uchunguzi aliokuwa ameuagiza ufanyike dhidi yake. 
 
Bwana Luhanjo alichukua hatua ya kumsimamisha Bw. Jairo kufuatia tuhuma zilizokuwa zimeelekezwa dhidi yake na baadhi ya wabunge wakati wa mjadala kuhusu Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2011/12 katika kikao cha Bunge kilichofanyika tarehe 18 Julai, 2011. Katika mjadala huo, baadhi ya wabunge walihoji uhalali wa Wizara kuomba michango ya fedha kutoka kwenye Taasisi zilizoko chini ya usimamizi wake ili kusaidia Bajeti ya Wizara hiyo kupita kwa urahisi. 
 
Kufuatia hatua hiyo ya kumsimamisha kazi Bw. Jairo, Katibu Mkuu Kiongozi alimwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bwana Ludovick Utouh kufanya ukaguzi maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhuma hizo. Tarehe 9 Agosti, mwaka huu, 2011, Bw. Utouh aliwasilisha Ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi, na tarehe 23, Agosti, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi akiambatana na Bw. Utouh alitangaza mbele ya waandishi wa habari matokeo ya ukaguzi huo maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhuma dhidi ya Bw. Jairo.
 
 
Katika Ripoti yake mbele ya waandishi wa habari, Bw. Utouh alihitimisha: “Ukaguzi maalum haukuthibitisha kuwepo kwa usahihi wa tuhuma zilizotolewa dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Kitundu Jairo.” Kufuatia Ripoti hiyo ya Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi naye aliwaambia waandishi wa habari: “Matokeo ya uchunguzi huo ni kwamba tuhuma zilizotolewa Bungeni tarehe 18 Julai, 2011, hazikuweza kuthibitika. "Kutokana na matokeo haya ya uchunguzi wa awali, mimi kama Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuu, Nishati na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na Hati ya Mashitaka kwa sababu Bwana David Kitundu Jairo, hajapatikana na kosa la kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi Maalum.
 
” Alihitimisha: “Kufuatia matokeo ya taarifa hii ya awali na kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibu wa Sheria Na. 8 ya Utumishi Umma ya Mwaka 2002 na kanuni zake za Mwaka 2003, NINAAMURU BWANA DAVID KITUNDU JAIRO AREJEE KAZINI KUANZIA SIKU YA JUMATANO, TAREHE 24 AGOSTI, 2011.” KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU, inapenda kutoa ufafanuzi kuwa baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi ya CAG na uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu suala hilo asubuhi ya tarehe 25 Agosti, 2011, 
 
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliamua kuwa Ndugu Jairo asirudi kazini mpaka kwanza yeye Rais atapoamua namna gani ya kurudi kazini, lini na wapi.Katibu Mkuu Kiongozi alifikisha uamuzi huo wa Rais kwa Ndugu David Jairo ambaye mapema asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameripoti kazini. Ndugu Jairo alitii uamuzi huo wa Rais. 
 
Tunapenda kusisitiza kuwa Mheshimiwa Rais hajawa kigeugeu kwa sababu alifanya uamuzi mmoja tu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Na uamuzi huo aliufanya kabla ya Bunge kulizungumzia suala hilo na hivyo uamuzi huo wa Rais haukutokana na shinikizo la Bunge. Pamoja na kumweleza Katibu Mkuu Kiongozi, Rais pia alimfahamisha Waziri Mkuu kuhusu uamuzi wake huo asubuhi hiyo ya tarehe 25, 2011. 
 
Aidha, tunapenda kufafanua zaidi kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ametimiza wajibu wake ipasavyo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Katibu Mkuu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Rais, kwa upande wake,ametumia madaraka yake kama Mamlaka ya Ajira ya Katibu Mkuu. Hakuna suala la kujichanganya wala ukigeugeu ndani ya Serikali kuhusu suala hili. 
 
Mwisho.
 
Imetolewa na 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,  
Ikulu, Dar es Salaam.
  26 Agosti, 2011

Friday, August 26, 2011

Corruption Nomaaaaa!!!!!

 Wananchi wa India wameendela kuikaba koo serikali yao kwa kashfa za Rushwa zifikiazo kiasi sawa na Tshs 320,000,000,000,000,000/=
ANNA HAZARE
Summary of All scams of India : Rs. 910603234300000/-
  NA MDAU WA 6000 PATSUNG

Thursday, August 25, 2011

Rais Jakaya Kikwete Amsimamisha Kazi Katibu Mkuu Nishati na Madini David Jairo

 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw David Jairo alipokua anazungumza na Waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuripoti wizarani jana.
Wafanyakazi kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma kwa nyuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo mapema jana asubuhi.
--
Habari toka Bungeni Mjini Dodoma zinasema Rais Jakaya Kikwete ameamuru  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Bw David Jairo asiendelee na kazi hadi hapo baada ya uchunguzi dhidi yake wa kuchangisha pesa ili Bajeti ya wizara yake ipite ukamilike.
Hayo yamesemwa sasa hivi na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda wakati akijibu swali la papo kwa hapo toka kwa Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe, ambaye alitaka kujua kama Bw. Jairo ataendelea kuwa likizo ili kupisha mchakato wa uchunguzi huo utaofanywa na kamati teule ya Bunge.
"Jambo hilo limekwisha fanywa na Mheshimiwa Rais", alijibu Mh Pinda kwa utulivu na kwa kifupi baada ya swali hilo,huku wabunge wakishangilia kwa kugonga meza. Hatua hii inakuja siku moja tu baada ya Bw. Jairo kuripoti ofisini kwa shangwe, ambapo wafanyakazi wa wizara walimpokea kwa vifijo, na wengine hata kusukuma gari lake hadi ofisini, aliporipoti mapema asubuhi.
Uamuzi wa kumrejesha kazini Bw Jairo ulipokewa kwa husia tofauti na  kila kada nchini, wengi wakihoji sababu ya mhimili mmoja kati ya mitatu iliyopo (Serikali, Bunge na Mahakama) kuingilia mwingine, ikizingatiwa kamba sakata hilo liilianzia bungeni na wengi walihisi ingekuwa vyema Bunge lingelishughulikia hadi mwisho.
Bunge lililidhia kuundwa kwa kamati maalumu kuchunguza tuhuma hizo na  inategemewa wajumbe wake watatangazwa kesho wakati wa kufunga kikao cha  Bunge kinachoendelea sasa. Ripoti yake inategemewa kutolewa Bunge lijalo
Na H@ki Ngowi

Crazy Yet Amazing Photo!!!!

Zoo performer Theerapone Manolai smiles as he puts his head between the jaws of a crocodile during a performance for tourists at the Sriracha Tiger Zoo, about 120 km (74 miles) east of Bangkok August 16, 2011. Kanthida Jantanct and Theerapone, both 28, from the province of Chaiyaphum, who have been crocodile performers at the zoo for almost ten years, earn at least 30,000 Baht (1,000 USD) per month for performing shows for at least 2,000.

VIONGOZI MBALIMBALI WASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU MUSSA HAMIS SILIMA

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi ya Viongozi, kubeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja jana.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif na baadhi ya viongozi wakiwa katika dua ya kumuombea aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Unguja, marehemu Mussa Hamis Silima, aliyefariki Agosti 23 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam, alikolazwa baada ya kupata ajali Agosti 22. Marehemu Silima amezikwa jana Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.
Waziri Mstaafu, Edward Lowassa,  akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja jana.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja jana.
Mwenyekiti wa Makati ya Bunge ya kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja jana.

 Rais wa Zanzibar,Dkt.  Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal,Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Mbunge wa Bumbuli na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January Makamba wakiwa katika shughuli ya maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Silima. Maziko hayo yamefanyika jana Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA