Rais
Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam, Meck Dadick, wakiomba dua kwa pamoja baada ya
kupata futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika makazi yake Oysterbay jijini jana, Agosti
27
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba
na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad saul, wakiwa
pamoja wakati wakisubiri muda wa swala kabla ya kupata futari
iliyoandaliwa na Makamu wa Rais katika makazi yake Oysterbay jijini Dar
es Salaam jana Agosti 27.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa
Rais, Sazi Salula, baada ya hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
katika makazi yake oystebay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.
Rais
Dkt. Jakaya kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakiagana na baadhi ya wananchi waliofika katika futari iliyoandaliwa na
mwenyeji wao Makamu wa rais katika makazi yake Yosterbay jijini Dar es
Salaam jana Agosti 27, ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru kwa kuhudhulia
hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya CXC Africa Ltd, Charles
Hamkah, wakati alipowaalika wageni katika hafla ya futari katika makazi
yake Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba, baada ya
kumalizika kwa hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu katika makazi
yake Oysterbay Dar es Salaam jana Agosti 27.
(Picha Zote na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais)
0 comments:
Post a Comment