ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT A LOWEST COST AND ALSO SEND TO US NEWS, EVENTS FOR MORE INFORMATION CONTACT US TELEPHONE: +919160901191 E-mail: ally.shaaban@yahoo.com | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA GHARAMA NAFUU NA PIA TUTUMIE HABARI, MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +919160901191 Barua Pepe: ally.shaaban@yahoo.com | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI HAPA

Saturday, July 30, 2011


Bajeti Ya Marekani  Imekwama!!!
Mjadala kati ya wanasiasa, kuhusu bajeti, na jinsi ya kuzidisha kiwango cha mkopo wa serikali ya Marekani ungali umekwama.
Ufumbuzi unatakiwa ufikiwe kabla ya Jumaane, ambapo Wizara ya Fedha itaanza kupungukiwa na fedha za kulipia matumizi ya serikali.
Ijumaa usiku, baraza la wawakilishi, ambalo wabunge wake wengi ni kutoka chama cha Republican, lilipitisha mswada kuzidisha kiwango cha mkopo na kupunguza matumizi ya serikali, lakini mswada huo ulikataliwa na baraza la Senate, lenye wajumbe wengi wa chama cha Democrat.
Hali ya uhasama na mashindano imetanda Washington huku Jumaane inakaribia.
Wanasiasa bado wanavutana wakati wanahitaji kupatana ili kuepuka wasi-wasi na pengine matafaruku katika uchumi wa Marekani, ikiwa muafaka haukufikiwa kabla ya tarehe ya mwisho, yaani tarehe mbili Agosti. 
Mswada uliopendekezwa na wabunge wa chama cha upinzani cha Republican Ijumaa, katika baraza la wawakilishi, ulizimwa katika baraza la Senate, ambako wajumbe wa chama cha Democrat sasa wanashindana na upinzani, na wanajaribu kusukuma mbele pendekezo lao wenyewe.
Lakini mswada huo piya, uliopendekezwa na kiranja wa chama cha Democrat, Harry Reid, unafanyiwa kazi ili ukubalike kwa wengi.
Vikao kati ya wanasiasa vitaendelea weekendi nzima na huenda makubaliano yakafikiwa dakika ya mwisho, na hatimaye kuwatuliza raia na masoko.

Wednesday, July 27, 2011

Mbunge wa Ilemela(Chadema)Ezekiel Wenje Atolewa Bungeni

Mbunge wa Ilemela-Cahdema, Mheshimiwa Ezekiel Wenje
--
Mbunge wa Ilemela kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ezekiel Wenje ametolewa nje ya Bunge katika leo  Mjini Dodoma.Mheshimiwa Wenje ametolewa nje ya bunge na Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba ambaye ndiye anayeongoza kikao hicho, baada ya kuvuana huku akihoji kuwa mwenyekiti huyo anaongoza kwa kuwaburuza wabunge.

Wakati Wenje akiwasha kipaza sauti kuzungumza tayari kulikuwa na mabishano yakiendelea kati ya Mbunge Moses Machali (NCCR-Magezi Kasulu Mjini) aliyekuwa akihoji muda mfupi aliokuwa amepewa mbunge wa CHADEMA, Tindu Lisu kuthibitisha kauli yake ambayo alidai mmoja wa mawaziri wenye dhamana na kodi amelidanganya bunge katika majibu yake.
Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo ya Wenje baada ya kutolewa nje anasema mbali na mabishano hayo alitaka kutoa taarifa ya uwepo wa taarifa za kuingia kwa samaki wa sumu nchini jambo ambalo ni hatari kwa wananchi.

Kitendo cha kutolewa kwa Mbunge Wenje bungeni hakikuwapendeza wabunge wa CHADEMA hivyo nao kutoka nje ya Bunge na  Kuzungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi huku bunge likiendelea bila ya wao kuwepo Bunge linaendela na Kikao Chake Jioni Hii

Mubarak Wa Misri "Agoma Kula"

Mubarak
Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak ni dhaifu na amegoma kula, kulingana na shirika rasmi la habari nchini humo.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo, akituhumiwa na makosa ya rushwa na kuamuru kufanyika kwa mauaji ya waandamanaji.
Bw Hosni Mubarak
Mkuu wa hospitali ambapo Bw Mubarak ameshikiliwa huko Sahrm al-Sheikh amesema alikuwa mnyonge, amepungua uzito, na hakuwa akila vya kutosha kumweka hai, shirika la MENA limeripoti.
Lakini wakosoaji wamesema ugonjwa wa Bw Mubarak ni kama njama ya kuepuka kufikishwa mahakamani.
Wafuasi wa upinzani wanatia shaka ripoti hiyo. Wanaamini mamlaka husika zinajaribu tu kuzuia kuanza kwa kesi ya Bw Mubarak, inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Miongoni mwa ripoti nyingi zilizotolewa kuhusu afya ya Bw Mubarak ya hivi karibuni imesema madaktari wake wataamua katika saa za hivi karibuni, iwapo ulaji wake wa hivi sasa hautoshi kumweka hai.
Mwandishi wa BBC Cairo, Jon Leyne, alisema, sasa hivi kuna ushahidi unaozidi kuibuka kwamba ni mtu anayedhoofika kadri siku zinavyoendelea.
Bw Mubarak alipinduliwa mwezi Februari katika ghasia maarufu zilizosababisha vifo vya zaidi ya watu 840.

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL,RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA,WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE WAONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU PROFESA MUSHI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa Samuel Mushi, wakati alipofika katika shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, pamoja na baadhi ya viongozi wakiwa katika shughuli ya mazishi na kuaga mwili wa marehemu  Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo 
Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Profesa Mushi, na ndugu jamaa na marafiki, wakiwa katika shughuli za mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika leo,kwenye ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick  Sumaye, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya marehemu Profesa Samuel Mushi, alipofika kuaga mwili katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu wa Rais

Mwili wa Mtoto Ally Rashid Shabani (7) Aliyegongwa na Gari na Kutupwa Ufukwe wa Coco, Dar es Salaam

Ndugu na majirani wakiwa wamebeba mwili wa mtoto Ally Rashid Shabani (7) aliyegongwa na gari na kutupwa ufukwe wa Coco, Dar es Salaam, wakiwasili nyumbani baada ya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam. Mazishi yalifanyika katika makaburi ya Mbuyuni Mtoni Relini, Dar es Salaam.Picha na Yusuf Badi

Saturday, July 23, 2011


Rais Jakaya Kikwete Akutana na Waziri Wa Afya na Huduma Za Jamii Wa Marekani

Rais Jakaya Kikwete (Kulia)na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhadrt wakishuhudia wakati Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Waziri wa Afya na Huduma za Jamiii wa Marekani  Bi Kathleen Sebelius Ikulu Jijini Dar es Salaam Jana.Mgeni huyo yupo nchini kwa Ziara ya Kikazi

Friday, July 22, 2011

MDAU AHMED MBARAK WA MJINI KHARKOV NCHINI UKRAINE ALA NONDOZZ !!!!!

Bachelor Degree of Economic-Computer Cybernetic. Awarded first Class Degree July18.2011 Kharkov. Ukraine. 
Bwana Ahmed Mbarak.
Bwana Ahmed na Mdau wa karibu(Best).
 Bwana Ahmed na Wakuu wa Kitengo katika picha ya pamoja.
Bwana Ahmed na Wadau.
Hapa Bwana Ahmed watatu toka kulia akiwa na Wakuu wa kitengo, na Wadau katika kuweka kumbukumbu.
Hapa Bwana Ahmed na Wadau wengine wakishangilia kumaliza masomo yao huku wakiashiria jamani mmeona........!! 
Habari na Picha  kwa niaba  ya Mdau wa 24 Seven 365 Bwana Ahmed Mbarak Ukraine.

Thursday, July 21, 2011

PINDA: HATIMA YA JAIRO IKO KWA RAIS


Rais Jakaya Kikwete.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameyaweka hadharani maagizo aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tuhuma za rushwa zinazomkabili Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akisema amemwambia kwamba atashughulikia suala hilo yeye mwenyewe atakapotoka ziarani Afrika Kusini.
Juzi, Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali bungeni, aliliambia gazeti hili kwamba alipewa maagizo na Rais juu ya kushughulikia tuhuma za kutenga zaidi ya Sh moja bilioni, kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.
Hata hivyo, jana alipoulizwa nje ya ukumbi wa Bunge kuhusu maelekezo hayo ya Rais, Pinda, alijibu: "Mheshimiwa Rais amesema atakuja kulishughulikia akirudi."
Pinda ambaye siku ya tukio hilo alionekana kuhamaki bungeni na kusema kwamba kama angekuwa na mamlaka angemfukuza kazi Jairo, jana alionekana mwenye subira huku akisisitiza kuwa: "suala hilo halina uharaka."
Tuhuma dhidi ya Jairo ziliibuliwa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ambaye alisema mtendaji huyo mkuu wa wizara alitoa dokezo kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kutoa Sh50 milioni ili kufanikisha bajeti kupita bungeni hatua ambayo iliibua hasira miongoni mwa wabunge hasa ikizingatiwa hali ya nishati ya umeme ilivyo kwa sasa nchini.
Shellukindo katika tuhuma zake alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma. Kabla ya ufafanuzi huo wa Pinda, jana mchana kulikuwa na tetesi zilizozagaa katika jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mitandao ya intaneti zikidai kwamba Jairo ameandika barua ya kuomba kujiuzulu. Akizungumzia tetesi hizo Pinda alisema: "Sina taarifa hizo," na kuongeza Pinda na kukiri kwamba hata yeye amezipata lakini haelewi chochote kuhusiana na hilo.
Jumatatu wiki hii, baada ya Shellukindo kuibua tuhuma hizo bungeni, Pinda aliahidi kuwa angewasiliana na Rais siku hiyo baada ya kutua kutoka kwenye ndege kwa ajili ya kumchukulia hatua za kinidhamu... "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.
Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.
Hata hivyo, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema haijui chochote kuhusu mawasiliano hayo ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda, kuhusu hatua za kushughulikia jambo hilo. Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga alisema hadi jana mchana, kurugenzi hiyo haikuwa na taarifa yoyote juu ya tuhuma zinazomhusu Jairo wala mawasiliano baina ya Waziri Mkuu na Rais.“Kama (Waziri Mkuu Pinda kumpigia Rais Kikwete), atakuwa amempigia siyo lazima sisi tujue,” 
alifafanua  Kibanga.
Chanzo: Click

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKUTANA NA MADEREVA TUNDUMA(BODA) KUZUNGUMZIA KUONGEZEKA KWA SIKU ZA KUSIMAMIA MAGARI MIZANI KUTOKA SIKU TANO HADI SABA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akifafanua jambo kwenye mkutano huo na madereva
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Mwakipesile akiwa amekasirika baada ya kukutana na maswali mengine yanayoonyesha kutokukubaliana na yale wanayoshauriwa!
Uongozi wa madereva pamoja na mkuu wa mkoa katikati na kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mbozi wakisikiliza jambo kutoka kwa madereva hao
Meneja wa TRA kitengo cha forodha bwana Rogacian Shirima akizungumzia kuongeza idadi ya siku za kusimamia magari hayo kutoka Dar hadi Tunduma ama Kasumulu ambapo watachukua siku saba badala ya siku tano za awali.
Kamanda wa polisi wilaya ya Mbozi Afande Ernest Dudu akizungumzia utaratibu Trafiki kukagua magari hayo tu pale yanapokuwa mizani.
Hapa viongozi wa madereva wa Magari ya biashara wakikataa  hivi hivi pale hoja yao ilipokumbana na upinzani wa wale wanaowaongoza

Sunday, July 17, 2011

HAPPY BIRTHDAY AHMED MBARAK

Bwana AHMED MBARAK 
Siku kama ya leo alizaliwa Mdau wa 24 SEVEN 365 anaitwa Bwana AHMED MBARAK, akiwa Masomoni katika Mjini wa KHARKOV Nchini UKRAINE anasomea Masuala ya ECONOMIC-COMPUTER CYBERNETICS. 
Blogu hii inaungana na Familia yake, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote katika kukutakia siku njema iliyo na Furaha, Amani na Upendo, na pia Mafanikio katika maisha yako. 
Mwenyezi Mungu akujaalie Afya Njema,Maisha Marefu, Busara na Hekima katika siku zote za maisha yako.
HAPPY BIRTHDAY AHMED MBARAK!! 

Thursday, July 14, 2011

Kenya Kufungua Kambi Ya Ifo II


Waziri Mkuu Raila Odinga
Serikali ya Kenya imeamuru kufunguliwa kwa kambi ya Ifo kaskazini mashariki mwa Kenya ambako maelfu ya watu wanawasili kila siku wakikimbia ukame na mzozo nchini Somali.
Amri hii imetolewa na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga aliyetembelea kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo ni kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani , ikiwahifadhi wakimbizi zaidi ya elfu mia tatu na mia nane, idadi ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa kambi hiyo.
Serikali ya Kenya ilikuwa imekabiliwa na shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kufungua kambi nyingine lakini ikawa na hofu juu ya usalama wa nchi na kuhofia kwa wakimbizi hao wakejenga makao ya kudumu nchini Kenya.

Saturday, July 9, 2011

10-Year-Old Willow Smith Is A Fashion Icon?

Will Smith's pop star daughter Willow has been named a fashion icon by top designer Derek Lam.
The 10-year-old "Whip My Hair" hitmaker and actress has been showing off her sassy style on the red carpet in recent months, and her bold and colorful wardrobe choices have caught the eye of California-based Lam, who has chosen Willow Smith has his top pick for Vogue magazine.
He describes the youngster as: "Naturally talented, charismatic, unblemished optimism, with the whole wide world open to her possibilities and abilities. I think she is the future-forward American icon."
Vogue editors asked a slew of designers to name their style picks and Smith is in good company - Brazilian supermodel Gisele Bundchen, actresses Michelle Williams and Cate Blanchett, model/filmmaker Christy Turlington and First Lady Michelle Obama all feature on the list.
Pop pair Taylor Swift and Katy Perry are also highlighted by Tommy Hilfiger, who says, "With Taylor's energetic charisma and Katy's edgy charm, they look as good in a casual summer dress as they do on the red carpet."

Michael Essien Aumia Goti Mazoezini


Michael Essien
Kiungo wa Chelsea Michael Essien ameumia goti alipokuwa mazoezini.
Taarifa ya klabu hiyo imesema: "Michael ameumia goti la mguu wake wa kuume mazoezini wiki hii.
"Atafanyiwa uchunguzi siku chache zijazo kutambua ukubwa wa tatizo lake. Hadi tutakapopata matokeo kamili, kwa sasa klabu haitakuwa na la kuongeza."
Essien mwenye umri wa miaka 28, mwaka 2008 hakucheza soka kwa muda wa miezi sita baada ya kuumia goti.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana pia alishindwa kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini kutokana na kuumia goti na kuumia kwake hivi sasa kunaonekana ni pigo kwa meneja mpya wa Chelsea Andre Villas-Boas, ambaye yumo katika kukinoa kikosi chake kwa ajili ya ziara ya Mashariki ya Mbali, ambapo timu hiyo itashiriki katika mashindano ya Kombe la Asia.
Wakati huo huo Chelsea imemtangaza Michael Emenalo kuwa mkurugenzi mpya wa michezo.
Emenalo alikuwa mwalimu msaidizi katika kikosi cha kwanza msimu uliopita, anachukua nafasi iliyoachwa na Ray Wilkins aliyehama klabu hiyo.
Mkurugenzi huyo mpya wa michezo kazi yake kubwa itakuwa ni katika mtandao wa kutafuta wachezaji wapya na maendeleo ya mipango ya wachezaji vijana na hali kadhalika kumsaidia Villas-Boas.

Sudan Kusini Nchi Huru


Sudan Kusini
Maelfu ya wananchi wa Sudan Kusini wamekusanyika kushuhudia kupandishwa kwa bendera mpya ya nchi hiyo kuashiria kupata uhuru wake, katika mji mkuu Juba.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki-moon ni miongoni mwa wageni waliohudhuria shughuli hiyo.
Sudan Kusini limekuwa taifa jipya duniani usiku wa kuamkia Jumamosi, lengo ambalo limefikiwa kufuatia mkataba wa amani wa mwaka 2005 uliomaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka mingi.
Sudan lilikuwa taifa la kwanza kuitambua Rasmi Sudan Kusini.
Uhuru wa Sudan Kusini unafuatia mzozo kati ya Kusini na Kaskazini uliosababisha vifo vya watu milioni 1.5.
Sherehe za uhuru zilianza saa sita kamili saa za Sudan Kusini mjini Juba. Saa iliyowekwa katikati ya jiji ilipotimu saa sita kamili, wimbo mpya wa taifa ulipigwa kupitia televisheni ya taifa hilo.
Sudan Kusini inakuwa taifa la 193, na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, na pia kuwa taifa la 54 barani Afrika.

Friday, July 8, 2011

Saa Chache Kuelekea Uhuru Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
South Sudan flag 
Sudan Kusini inahesabu saa chache ili kuwa Taifa jipya kabisa kuzaliwa duniani Jumamosi ya Julai 9.Rais wa Sudan Omar al-Bashir na wageni wengine mashuhuri kutoka kote duniani watahudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika mji mkuu Juba.Zaidi ya asilimia 99 ya Wasudan Kusini walipiga kura kujitenga na Sudan Kaskazini katika kura ya maoni iliyofanyika mwezi Januari.Kura hizo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2005 kumaliza miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha watu 1.5 milioni kufa.Nchi mpya ya Sudan itakuwa na utajiri wa mafuta lakini itakuwa moja ya nchi maskini kabisa duniani kutokana na mapigano ya muda mrefu.Sherehe zitaanza baada ya saa sita usiku saa za Sudan (2100 GMT) kwa kuhesabu dakika chache kufikia saa kamili ya kuwanza kwa siku wakitumia saa kubwa katikati mwa Juba.Mwandishi wa BBC Will Ross anasema katika kuelekea kwenye tukio hilo la kihistoria, vituo vya redio vimekuwa vikipiga wimbo mpya wa Taifa la Sudan Kusini.
Mapema wiki hii Bw Bashir aliahidi kuiunga mkono Sudan Kusini na kusema kuwa anataka Taifa hilo jipya kuwa ‘salama na lililotengamaa."Tutawabariki ndugu zetu wa Kusini nchini mwao na tunawatakia mafanikio" alisema Bw Bashir, aliyekubaliana na mkataba wa amani na chama cha Sudan People's Liberation Army (SPLA).Lakini ameonya kuwa ‘Uhusiano wa kindugu’ utategemea na mipaka salama na kutoingilia masuala ya nchi jirani (Kusini au Kaskazini)"Kwa hiyo tunafuraha sana na tunashukuru kwa mchango ao kwa Taifa hili."Rebecca Garang, mke wa hayati John GarangKulikuwa na wasiwasi huenda vita vingezuka tena baada ya mapigano mapya ya hivi kribuni katika maeneo ya mpakani Abyei na Kordofan Kusini ambayo yalilazimisha watu 170,000 kukimbia makazi yao.Hata hivyo makubaliano tofauti ya wiki za hivi karibuni na kuondoa vikosi kwenye mipaka kumerejesha hali ya utulivu.Rebecca Garang, mke wa hayati John Garang aliyeongoza waasi wa Sudan katika vita vya wenyewe kwa wenyewe , ameiambia BBC kuwa watu wake hawana matatizo na watu wa Kaskazini isipokuwa serikali yao."Kuna rafiki zetu wengi tu ambao walikufa wakati w vita lakini tuko hapa kwa ajili ya damu yao," alisema.
For more: Click 

Thursday, July 7, 2011

HAPPY BIRTHDAY TO YOU

 FOIBE J. MCHOME
 ABDULKARIM AFTAB (THE GREAT)
MAY ALMIGHT GOD BLESS YOU WITH A GOOD HEALTH AND LONG LIFE.

Wednesday, July 6, 2011

Timu Ya Wabunge iliyoongozwa na Naibu Spika Job Ndugai Kufwatilia Hukumu ya Malipo ya Rada Kutoka Kampuni ya BAE ya nchini Uingereza Yawasilisha Ripoti Yake Kwa Spika Anne Makinda Leo

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda  akionyesha kwa waandishi wa habari ripoti ya timu ya Bunge kuhusu ufuatiliaji wa hukumu ya malipo ya rada kutoka kwa kampuni ya BAE ya nchini Uingereza. Mkutano huo na waandishi wa habari umefanyika leo (jana) Bungeni mjini Dodoma
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda akipokea ripoti ya timu ya wabunge wa Bunge la Muungano wa Tanzania kutoka kwa Kiongozi wa timu hiyo ambaye ni Naibu Spika Mhe. Job Ndugai. Timu hiyo  ilikwenda nchini Uingereza kufuatilia hukumu ya malipo ya fedha za rada kutoka katika ya British Aerospace (BAE ) ya nchi humo ambayo inadaiwa na Serikali ya Tanzania kiasi cha zaidi ya Tsh. Bilioni 80. Mkutano huo na waandishi wa habari umefanyika leo (jana) Bungeni mjini Dodoma.
KIONGOZI wa timu ya Bunge iliyofuatilia hukumu ya malipo ya rada ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Job Ndugai (katikati) akitoa taarifa ya ujumbe wa timu hiyo katika ukumbi wa mikutano Bungeni mijini Dodoma. Kulia kwake ni mjumbe wa timu Mhe. Angela Kairuki (Viti Maalum) na kushoto ni Mussa Azzan Zungu (Ilala).
Picha zote na Islamail Ngayonga-MAELEZO.

Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu Anyakua Taji La Miss Southern Afrika International 2011

Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu akiwa na shada la maua muda mfupi baada ya kuwasili nchini
Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu akiwa katika pozi
Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu(kushoto)akipokewa na Maria Sarungi Muda Mfupi baada ya Kuwasili.
**************
Mrembo aliyeshinda taji la Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu ameshinda taji la Miss Southern Afrika International 2011 katika mashindano yaliyofanyika Ndola nchini Zambia na kushirikisha warembo kutoka nchi mbalimbali za kusini na mashariki mwa Afrika.Nelly aliyepata mwaliko wa kushiriki mashindano hayo kupitia bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ameshinda taji hilo jumapili ya Juni 27 mwaka huu.
Fursa hiyo imemsaidia Nelly kupata uzoefu kabla ya kwenda katika mashindano ya Miss Universe kimataifa mwezi wa nane na tisa mwaka huu.Mashindano hayo mbali ya kujenga mshikamano miongoni mwa nchi za kiafrika yanalenga pia kuvutia na kutangaza utalii wa nchi washiriki.
Mbali na kuhsiriki shindano la urembo,wakiwa nchini Zambia warembo washiriki akiwemo Nelly walihsiriki na kufanya kazi mbalimbali za kijamii kama vile kutembelea hospitali za watoto na vituo vya kulelea watoto na kushiri maonyesho ya kimataifa ya biashara nchini humo.
Ukiondoa Tanzania nchi nyingine za Afrika zilizoshiriki ni Namibia, Zambia, Lesotho,  Afrika ya Kusini, Botswana, Zimbabwe, Swaziland, Congo, Malawi na Msumbiji.Nyota ya Nelly ilianza kung’ara pale aliposhinda taji la Miss Universe katika shindano lililodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ikiwa ni sehemu ya azma ya kampuni hiyo ya kuibua,kuendeleza na kulinda vipaji vya vijana wa kitanzania katika sanaa na michezo.
Azma hiyo inalenga kuwapatia fursa vijana ya kujiendeleza kimaisha kupitia vipaji pamoja na kutimiza ndoto walizonazo katika sanaa.Kwa kushikilia taji la Miss Southern Afrika Internation Nelly anawajibu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya saratani ya matiti na mfuko wa uzazi na atakuwa balozi wa nia njema wa mtandao wa saratani ya matiti na mfuko wa uzazi Zambia.
Aidha ushindi huo umempatia Nelly pamoja na zawadi mbalimbali mshahara wa kwacha millioni moja kwa mwezi kwa kipindi cha miezi kumi na minne.
Kwa Hisani ya H@ki Ngowi.

Ombi La Liverpool Lakataliwa Na Villa

Stewart Downing mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa
Klabu ya Aston Villa, imekataa ombi la Liverpool la kuitaka kumsajili mchezaji wake Stewart Downing kwa kitita cha £15m.
BBC imegundua kuwa klabu ya Aston Villa, inataka kulipwa kitita cha £20m ili kukubali uuzaji wa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza mwenye umri wa miaka 26.
Stewart ambaye alijiunga na Villa kutoka kwa klabu ya Middlesbrough kwa kitita cha £12m mwaka wa 2009, hajaafikiana na kocha wake Alex McLeish kuhusu kandarasi mpya na duru zinasema kuwa kocha huyo yuko tayari kumuuza stewart.
Mchezaji huyo wa kiungo cha kati pia amehusishwa na klabu ya Arsenal, lakini Liverpool ina nafasi nzuri ya Kumsajili.
Habari zaidi zinaendelea kujitokeza.

Monday, July 4, 2011

Rais Jakaya Kikwete Azindua Rasmi Barabara ya Mwandiga-Manyovu Yenye Urefu wa Km 60

Rais Jakaya Kikwete akipokewa na mamia ya wananchi wa Mwandiga waliofurika katika sherehe za ufunguzi wa barabara.
 Rais Kikwete akizindua rasmi barabara ya Mwandiga-Manyovu yenye urefu wa km 60 iliyoko mkoani Kigoma tarehe 4.7.2011.
 Rais Kikwete akikata utepe na kufungua pazia kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwandiga-Manyovu yenye urefu wa km 60 iliyoko mkoani Kigoma tarehe 4.7.2011.Picha zote na John Lukuwi

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL USO KWA USO NA MAALIM SEIF SABASABA BAADA YA KUZINDUA GS 1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi huduma mpya ya Mfumo wa Utambuzi wa Bidhaa Tanzania, (Global Standard 1 ), wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere leo Julai 04, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Huduma Global Standard GS1 nchini Tanzania, ‘Mfumo wa utambuzi wa Bidhaa’Uliozinduliwa leo Julai 04, 2011 kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Dar es Salaa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa leo Julai 04, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Biala, akisikiliza maelezo ya mjasiliamali, Angela John, kuhusu mashine ya Kusokota, wakati alipotembelea katika Banda la Sido kwenye Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Power Electronics & Controls Ltd, Kayungi Kayungi, kuhusu Mashine ndogo inayozalisha Umeme kwa kutumia maji, wakati alipotembelea Banda la Sido kwenye Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam. 
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu wa Rais
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUSOMA HABARI ZILIZOPITA BOFYA NENO OLDER POSTS HAPO JUU ASANTE SANA KWA KUTEMBELEA NA KARIBU TENA