Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel
Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za
maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu
Profesa Samuel Mushi, wakati alipofika katika shughuli ya kuaga
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, pamoja na baadhi ya
viongozi wakiwa katika shughuli ya mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo
Baadhi
ya wanafamilia ya marehemu Profesa Mushi, na ndugu jamaa na marafiki,
wakiwa katika shughuli za mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa
Samuel Mushi, iliyofanyika leo,kwenye ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, nje
ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel
Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick Sumaye,
nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa
Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo. Katikati ni Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwafariji wanafamilia ya marehemu Profesa Samuel Mushi, alipofika
kuaga mwili katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo.Picha na
Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu wa Rais
0 comments:
Post a Comment