Mbunge wa Ilemela-Cahdema, Mheshimiwa Ezekiel Wenje
--
Mbunge
wa Ilemela kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Ezekiel Wenje ametolewa nje ya Bunge katika leo Mjini
Dodoma.Mheshimiwa Wenje ametolewa
nje ya bunge na Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba ambaye ndiye
anayeongoza kikao hicho, baada ya kuvuana huku akihoji kuwa mwenyekiti
huyo anaongoza kwa kuwaburuza wabunge.
Wakati Wenje akiwasha kipaza sauti kuzungumza tayari kulikuwa na mabishano yakiendelea kati ya Mbunge Moses Machali (NCCR-Magezi Kasulu Mjini) aliyekuwa akihoji muda mfupi aliokuwa amepewa mbunge wa CHADEMA, Tindu Lisu kuthibitisha kauli yake ambayo alidai mmoja wa mawaziri wenye dhamana na kodi amelidanganya bunge katika majibu yake.
Hata
hivyo kwa mujibu wa maelezo ya Wenje baada ya kutolewa nje anasema
mbali na mabishano hayo alitaka kutoa taarifa ya uwepo wa taarifa za
kuingia kwa samaki wa sumu nchini jambo ambalo ni hatari kwa wananchi.
Kitendo
cha kutolewa kwa Mbunge Wenje bungeni hakikuwapendeza wabunge wa
CHADEMA hivyo nao kutoka nje ya Bunge na Kuzungumza na waandishi wa
habari nje ya ukumbi huku bunge likiendelea bila ya wao kuwepo Bunge
linaendela na Kikao Chake Jioni Hii
0 comments:
Post a Comment