Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo kikuu cha TEKU akielezea kilicho wafanya wafike eneo hilo la kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Jeshi la polisi likiwa katika ulizi mkali wakati wanafunzi hao wakiwa ofisi za mkuu wa mkoa Mbeya
Wanachuo cha Teku Wakielekea ofisi za Mkuu wa mkoa jijini Mbeya
Wanachuo hao wakiwa wanahasira kali huku wakingojea majibu kutoka kwa wawakilishi wao ambao waliingia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya
Hili ni Bango ambalo linaelezea hisia zao za kutaka malipo.
************
Na Mwandishi wetu Joseph Mwaisango
WANACHUO 4500 wanaosoma katika chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU) kinachomilikiwa na Kanisala la Moravian Tanzania kilichopo Jijini Mbeya wamendamana mpaka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya kueleza yanayowapata baada ya kukosa mikopo yao.
Maandamano hayo yaliyoanzia chuoni hapo yalidumu kwa muda wa dakika 37 mpaka kufika ofisi hiyo ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambapo walipokaribia walizuiwa na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi kikiwa ndani na nje ya magari PT 2079 na PT 0796.
Baada ya kuzuiwa wanachuo hao ambao walifanya maandamano ya Amani waliwaambia waandishi wa habari waliofika eneo hilo kuwa nia yao ni kumweleza Mkuu wa mkoa Abbas Kandoro ama ofisi yake juu ya kukwama kwa jitihada zao za kufuatilia mikopo hiyo.
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Ambukege Imani alisema kuwa wanachuo hao walifanya jitihada za kupata kibali juzi kupitia jeshi la polisi ambalo lilikataa kuwapatia kibali hicho, na kwamba zaidi wanachuo hao wameshitushwa na taarifa iliyotoka bodi ya mikopo kuwa hawataweza kuwapa mikopo yao mpaka ifikapo mwezi Desemba 12 mwaka huu.
‘’Tulifanya jitihada za kuomba kibali cha maandamano lakini Polisi walikataa na viongozi wachache tulipoamua kuja kumuona Mkuu wa mkoa wenzetu wamekataa kubaki ndiyo maana wamefika hapa lakini yote ni kudai haki na tatizo ni majibu tunayoyapata kutoka bodi ya mikopo’’ alisema Rais Huyo.
Naye Waziri wa mikopo wa chuo hicho Mwilenga Lucas alisema kuwa kutokana na kucheleweshewa mikopo hiyo wanachuo wana hali mbaya ya kimaisha hivyo majibu yasiyoridhisha kutoka bodi ya mikopo ndiyo yanawalazimisha wanachuo hao kufikia hatua hiyo ya kutaka kujua ni nini kinaendelea.
0 comments:
Post a Comment