SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 17, 2011

Kutoka Saluni Hadi Uigizaji Nyota


Ukiona vyaelea, vimeundwa’ huu ni moja kati ya misemo iliyopo katika lugha ya Kiswahili ambayo inalenga kuonesha kuwa kila king’aacho au kila chenye mafanikio, kina mwanzo wake. 
Usemi huu utaweza kuakisi tasnia ya filamu hapa nchini ambayo baadhi ya wasanii wake wanang’ara na kuwa na mafanikio hivi sasa, lakini wakiwa na historia ya kuanza mikikimikiki mbali huku wakipitia mabonde na milima. 
Baadhi ya wasanii ambao kwa sasa wanang’ara lakini wamepita safari ndefu ni Steven Kanumba ‘Kanumba’, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven ‘JB’, Yvonne Cherrie ‘Monalisa’, Lucy Komba na wengineo wengi. 
Lakini pia wapo walioanza kuibuka ndani ya miaka takribani mitano iliyopita lakini kwa sasa wamekuwa tishio katika fani hiyo, mmojawapo ni msanii Jacqueline Wolper, ambaye karibu miaka minne, amekuwa mwigizaji nyota wa filamu kutokana na kazi zake kukubalika ipasavyo. 
Akizungumza katika mahojiano na HABARILEO Jumapili, Jackline ambaye anazungumza taratibu na kwa kituo na kama ni mtu wa kukurupuka unaweza kumdhania kuwa ana maringo, anaeleza nia yake ya kutaka kuwekeza katika fani hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wasanii wachanga. 
“Pamoja na mafanikio niliyoyapata ndani ya miaka minne, nina kiu ya kujidhatiti katika fani hii. Kiu yangu ni kuhakikisha nafungua kampuni kubwa ya kuuza vifaa vinavyotumika katika filamu, usambazaji wa kazi za filamu na kuanzisha kikundi cha sanaa. 
“Napenda sana kuwasaidia na kuwainua wasanii chipukizi kama mimi nilivyoinuliwa, na njia pekee ni kuwa na kikundi amchacho ndicho kitakachokuwa chimbuko la kuibua vipaji vya uigizaji,” anasema. 

0 comments:

Post a Comment