SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, September 7, 2011

Balozi Seif idd:Serikali itafwatilia Mwenendo Wa Biashara Ya Karafuu

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kushuhulikia Mashamba ya Serikali,  ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Mhe, Balozi Seif Ali Iddi akiwa na ujumbe wake walipotembelea kambi ya uchumaji wa zao la Karafuu ya Bw. Salum Mbaruku Salum iliyopo Kijiji Cha Ngwachani, Mkoa wa Kusini Pemba, Kamati nzima ya kushughulikia Mashamba ya Serikali ipo Kisiwani Pemba kwa ziara maalum.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe, Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa kushughulikia Mashamba ya Serikali, akikagua Karafuu za mkulima Bw, Ali Salim Ali wa Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba aliyekutwa akizichambua tayari kwa mauzo katika Shirika la Taifa La Biashara la Zstc
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe, Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia Mashamba ya Serikali akikagua zao la Karafuu ambazo tayari zimeshanunuliwa na Shirika la Zstc zikiwa Ghala kuu la Mkoani.

0 comments:

Post a Comment