Mnara wa Kumbukumbu.
Leo imetimia miaka 15 tangu itokee ajali ya meli ya abiria na mizigo ya MV BUKOBA, tarehe 21 May 1996 liyozama katika Ziwa Victoria. Na kusababisha Ndugu, Jamaa na Watanzania wenzetu zaidi ya 1,000 na kupotea na mali zao pia.
Kumbu kumbu hii inaturudisha nyuma hadi mwaka 1996 wakati meli hiyo ikisafiri kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza ndipo ilipokumbwa na ajali hiyo ikiwa umbali wa kilomita 56 kufikia bandari ya Mwanza na kutusabishia majonzi makubwa ambapo tulipoteza ndugu zetu wapendwa
Tunakumbuka jinsi wakati huo rais wa awamu ya tatu Ndugu Benjamini Mkapa alipotangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia maafa hayo.
Kama waungwana tunachukua fursa hii kuwafariji na kuwapa pole tena wale wote waliopoteza wapendwa wao tukiwaambia kuwa tuko pamoja nanyi katika kipindi hiki cha kumbukumbu.
Tunakupa pole wewe mpendwa ambaye siku kama ya leo ulimpoteza ndugu, mzazi, jamaa, rafiki yako kipenzi katika ajali hiyo,
Mungu akupe nguvu wewe pamoja na familia yako pamoja na wananchi wengine wote wa Tanzania na nje ya nchi wanaokumbuka machungu kama wewe.
Tunakupa pole wewe mpendwa ambaye siku kama ya leo ulimpoteza ndugu, mzazi, jamaa, rafiki yako kipenzi katika ajali hiyo,
Mungu akupe nguvu wewe pamoja na familia yako pamoja na wananchi wengine wote wa Tanzania na nje ya nchi wanaokumbuka machungu kama wewe.
Ni imani yetu kuwa roho za wapendwa wetu hao zimepumzika kwa amani mahali pema peponi.
Kwetu pamoja na kuwa ni siku ya kuwakumbuka wale tuliowapoteza lakini zaidi pia kwetu ni siku ambayo ni kengele kwa serikali kukumbuka suala zima la kuhakikisha usalama katika vyombo vya usafiri majini ikiwemo kuhakikisha tahadhari zote za kiusalama zinachukuliwa kabla ya chombo chochote kung’oa nanga ili majanga ya aina hii yasijirudie tena.
REST IN PEACE WOTE MLIOTUTOKA.
REST IN PEACE WOTE MLIOTUTOKA.
0 comments:
Post a Comment