Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki (kulia) pamoja na baadhi ya viongozi, wakiwa kwenye shughuli ya mazishi wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, Sheikh Yahya, aliyefariki dunia jana jijini na anatarajia kuzikwa leo kwenye makaburi ya Tambaza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(kushoto) akijumuika na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu kuomba dua
maalum kwa ajili ya marehemu Sheikh Yahya Husein, aliyefariki dunia
jijini Dar es Salaam jana,dua hiyo ilifanyika nyumbani kwa marehemu
Magomeni Mwembechai leo Mei 21. Maziko yatafanyika kwenye makaburi ya
Tambaza leo. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali mjane wa marehemu Sheikh Yahya, Kate Yahya, wakati
alipofika nyumbani kwake Magomeni Mwembechai leo Mei 21 kuhudhuria
shughuli za mazishi.
Baadhi
ya wanafunzi waliofundishwa na Marehemu Sheikh Yahya, wakiwa kwenye
shughuli za mazishi nyumbani kwa marehemu Magomeni Mwembechai leo Mei
21.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiondoka nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya Husein, baada ya kuhudhuria shughuli za mazishi leo Mei 21, Magomeni Mwembechai Dar es Salaam.
(Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
0 comments:
Post a Comment