SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 21, 2011

WAPINZANI WAITISHA MAANDAMANO YEMEN

Makundi ya wapinzani nchini Yemen yameitisha maandamano makubwa baada ya kuzuka tena kwa mapigano kati ya waandamanaji na polisi ambapo mtu mmoja ameuawa.
Watu wengine watatu wamekufa kutokana na majeraha waliyoyapata wakati wa maandamanao hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa mjini Sanaa.
Mazungumzo kati ya wapatanishi wa nchi za Ghuba na wawakilishi wa serikali ya Rais Ali Abdullah Saleh pia yanaonekana kutopata mafanikio yoyote.
Jumanne iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilimaliza kikao chake kilichokuwa kikiijadili Yemen bila ya kutoa taarifa rasmi.
Na Mo Blog

0 comments:

Post a Comment