Tamasha La Serengeti Fiesta Soka Bonanza Lafana Jijini Mwanza Jana
Mratibu wa Bonanza hilo Shafii Dauda wa pili kutoka kushoto akiongea na mashabiki kabla ya kukabidhi vikombe kwa washindi wa bonanza hilo, kushoto ni Khalfan Ngasa.
Mratibu wa Bonanza hilo Shafii Dauda wa pili kutoka kushoto akiongea na mashabiki kabla ya kukabidhi vikombe kwa washindi wa bonanza hilo, kushoto ni Khalfan Ngasa.
Hapa kikosi cha Real Madrid wachezaji wa timu hiyo kikiwa na kombe lao mara baada ya kukabidhiwa.
Timu ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Hispania wa jijini Mwanza imeibuka na ushindi wa jumla katika Tamasha la Mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililokutanisha mashabiki wa vilabu mbalimbali vya Barani ulaya, ambalo limefanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza baada ya kuwafunga mashabiki wa timu ya Chelsea ya Uingereza.

Mashabiki wa timu ya Chelsea ya Uingereza wakiwa na kombe lao mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika bonanza hilo.
Mashabiki wa Arsenal. Mmoja wa Waratibu wa Serengeti Fiesta soka bonanza,Abdul akiwa kwenye mchakato mzima mapema hii asubuhi jijini Mwanza kuelekea CCM Kirumba.
Golden Moment ya dereva Tax huyu ni pale alipokutana na Mratibu wa Serengeti Fiesta Soka Bonanza 2011,Shafii Dauda na kumpa kibeji cha Man U atie saini yake kama uonavyo pichani.
Jsehi la polisi limetoa msaada mkubwa kwenye maandamano haya ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza katika suala la zima la usalama barabarani,kama umuonavyo askari huyu wa usalama barabarani akiongoza maandamano hayo mapema jana asubuhi jijini Mwanza.
Mashabiki wa vilabu mbalimbali za nje,wa jijini mwanza wakiwa wameandamana mapema asubuhi kwenye mchakato mzima wa kuelekea uwanja wa CCM Kirumba,ambapo ule msimu wa Fiesta Bonanza na Serengeti ikiendelea kurindima,ambao msimu huo umeanzia jijini Dar na sasa ndani ya jiji la Mwanza jana.
Foleni ya magari yakiwa yamesimama, kuyapisha maandamano ya Serengeti Fiesta soka bonanza mapema jana asubuhi jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment