Kituo cha Televisheni ya Taifa ya Yemen imetangaza kuwa Rais Ali Abdullah Saleh wa nchi hiyo, amekubali kujiuzulu katika kipindi cha siku 30 na kumkabidhi madaraka msaidizi wake. Amekubali pendekezo lililotolewa na wasuluhishi kutoka nchi za Ghuba ya kupewa hifadhi, badala ya kushtakiwa pale atakapojiuzulu.
Rais Saleh anatawala tangu miaka 32 na anang'ang'ania kubakia madarakani, licha ya kukabiliwa na maandamano ya miezi miwili kupinga utawala wake. Wapinzani wake nchini humo wanamtaka, Rais Saleh ajiuzulu moja kwa moja na wanapinga kipengele kimoja katika makubaliano kuwa bunge lina haki ya kupinga rais kujiuzulu.
Wengi wa wabunge hao ni wanachama wanaotokea chama cha Rais Saleh.
Na Mo Blog.
0 comments:
Post a Comment