Mawaziri wa Nje kuijadili Libya
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka duniani kote wanakutana mjini Geneva Uswisi, kujadili hatua za kuchukua kukabiliana na janga la kibinaadam linalozidi kukua nchini Libya.
Waandamanaji Libya karibu na picha ya Gaddafi
Maelfu ya wahamiaji, wengi kutoka Misri, wamekwama katika mpaka wa Libya na Tunisia, huku maelfu wakiwasili kila saa, kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa.
Waandishi wa habari wanasema kuna hali ya wasiwasi, huku kiongozi Muammar Gaddafi akiendelea kuidhibiti Tripoli.
Wakimbizi kutoka Libya
Marekani imeunga mkono wazi wazi makundi yanayompinga Gaddafi mashariki mwa Libya.
Akifungua mkutano mjini Geneva, Kamishna wa haki za binaadam wa Umoja wa Mataifa Navi Pallay, amezionya mamlaka za Libya kuwa ushambuliaji wa raia unaotapakaa, unaweza kufikia kuwa makosa ya jinai katika sheria za kimataifa.
"Ni suala la masikitiko makubwa kwamba damu imemwagika katika kukaribisha mabadiliko".
Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo kwa Gaddafi
Akizungumza akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema Marekani "inaungana na wananchi wengi wa Libya wa upande wa mashariki".
Bi Clinton amesema atajadili masuala ya kibinaadam na kisiasa na mawaziri wengine kutoka Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika kaskazini katika mkutano wa baraza la haki za binaadam, mjini Geneva.
Watu wasiopungua 1,000 wanadhaniwa kuawa katika wiki mbili za ghasia, ambapo miji ya mashariki imedhibitiwa na majeshi yanayopinga serikali.
0 comments:
Post a Comment