SERIKALI YA SWEDEN YATOA MSAADA WA SH. BILIONI 44 KWA TANZANIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Kijjah (kushoto) akizungumza kabla ya kutia saini. Kulia ni Kiongozi wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden, Erik Korsgren.
SERIKALI ya Sweden imetoa msaada wa Sh. Bilioni 44 kwa Tanzania kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha huduma za usambazaji umeme vijijini zinazotekelezwa na mfuko wa usambazaji wa umeme vijijini (REA).Hadi sasa REA imepeleka umeme katika wilaya 11 na wanaendeleza shughuli hizo katika mikoa 16 nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Kijjah kwa pamoja na Kiongozi wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden, Erik Korsgren walisaini makubaliano ya kusaidia mradi huo wa umeme vijijini, katika hafla iliyofanyika jana Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Kijjah alisema serikali hiyo imekubali kuisaidia Tanzania ili kuwezesha REA kupanua na kutekeleza shughuli za umeme vijijini.
Picha na Vicent Tiganya
0 comments:
Post a Comment