Kipindupindu yawaua 540 - Haiti
Cholera yawaua watu Haiti
Madaktari katika mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, wamesema mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umetokea mjini humo ingawa hapajakuwa na thibitisho rasmi. Zaidi ya watu 540 wameaga dunia kufuatia maradhi hayo na wengine takriban 8000 wanapokea matibabu hosipitalini.
Kuna wasiwasi kwamba maradhi hayo huenda yakasambaa kwa haraka katika kambi za mji wa Port-au-Prince zinazowasitiri waathiriwa wa tetemeko la ardhi lililotokea mwezi Januari mwaka huu.
Juhudi za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo zinavurugwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga cha Tomas kilichopiga haiti mwishoni mwa juma.
0 comments:
Post a Comment